Header Ads

Breaking News
recent

MTUME WA MITUME AZURU TANZANIA


Mtume mkuu wa kanisa jipya la Mitume duniani leo atatua Jijini Mbeya na kuhubiri



Mtume mkuu wa kanisa jipya la mitume Duniani Wilhelm Leber.

Mtume huyo atahubiri maelfu ya waumini wa kanisa hilo katika ukumbi wa chuo kikuu cha Teofilo Kisanji kinachomilikiwa na kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini Magharibi lililopo Jijini Mbeya.

Taarifa za uhakika kutoka kwa mitume na Makuhani wa kanisa hilo zimeuambia mtandao huu wa www.msasawawiki.blogspot.com kuwa Mtume mkuu huyo katika ziara yake nchini Tanzania atahubiri katika mikoa miwili tu ukiwemo mkoa wa Mbeya na mkoa wa Mwanza ambapo Star TV itarusha moja kwa moja mahubiri hayo atakapokuwa Jijini Mwanza.

Kikosi kazi cha mtandao huu tayari kimetua katika eneo la tukio katika chuo cha TEKU Mbeya hivyo endelea kutembelea mtandao huu
Kwa hisani ya www.kalulunga.blogspot.com




No comments:

Powered by Blogger.