Header Ads

Breaking News
recent

KWANEEMA FM

Kwa Neema Fm ni kituo cha redio cha Kikristo chenye maono ya Kuhubiri habari njema za Ufalme wa Mungu  kwa watu wote na ni Kituo kinachopatikana katika masafa ya 98.1 MHz yakiwa ni matokeo makubwa ya maono ya Kanisa la Tanzania Field Evangelism chini ya Mtumishi wa Mungu Balozi wa Ufalme Bishop Dokta Augustine Mpemba.

Baada ya juhudi kubwa na kujitoa kwa mali na maombi kanisa lilipewa kibali cha kufungua redio ya Kwa Neema Fm chini ya kifungu cha 13 cha sheria ya Vyombo vya Habari mnamo tarehe 11/3/2010.
Mnamo Julai 03 2010 jiwe la msingi liliwekwa naye Askofu Mkuu wa kanisa la Crossroad la huko Marekani ambapo hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini, siasa na wa taasisi zisizo za kiserikali.   

Kuanzishwa kwa redio ya kwa neema kumebebeba misheni kubwa ya  kuhubiri uhitaji mkubwa wa mwanadamu kuacha maisha ya dhambi ili akombolewe na kufunguliwa kutoka katika minyororo ya Shetani kwa kutumia Maandiko Matakatifu ya Biblia.

Kwa Neema Fm inatumia jukwaa hilo la hewani katika Kushuhudia na kulitangaza Jina la Yesu Kristo,Kumhubiria mwanadamu kuacha maisha ya dhambi na Kutangaza kwa jamii kubadili tabia zisizofaa zinazopelekea maambukizi ya VVU/UKIMWI na Kuhabarisha  na kuelimisha kwa kutumia habari za kijamii na kimaadili kwa maendeleo umma.

Kwa Neema Fm redio inaheshimu watu wote wa dini na madhehebu mbalimbali na inaamini katika neema ya Yesu kristo iliyoaachiliwa kwa watu wote.

Pamoja na hayo yote Kwa Neema fm redio inatoa mafundisho yenye nia ya kubadilisha maisha ya watu katika mtazamo wa Kiroho, kinafsi na kimwili ili kuijenga jamii yenye afya kijamii, kimaadili, kisiasa na pia kiuchumi.

Baada tu ya kuanza kurusha matangazo yake Kwa Neema Fm redio imejijengea kiasi cha wasikilizaji milioni moja na nusu ikiwa inafika wilaya mbili za Mwanza mjini ambayo ni Ilemela na Nyamagana, pia Nansio Ukerewe, wilaya ya Sengerema, Magu, Misungwi na Kwimba lakini pia inasikika katika Mkoa wa Geita, Shinyanga Kahama, Mara Bunda, Musoma vijijini na wilaya ya Mugumu.

Kikiwa na miaka saba ya utendaji kazi kwa  mkoa wa Mwanza na maeneo jirani tumeshuhudia watu wakiokoka,kuponywa, kufunguliwa na kukua kiufahamu katika mambo ya Kiroho na maisha ya jamii yakibadilishwa katika wema.

Kwa namna ya ajabu shuhuda  nyingi zimekuwa zikitolewa na watu wa madhehebu mbali mbali kuhusu redio hii ilivyobadilisha maisha yao kupitia vipindi vya mafundisho  ya kiroho na kijamii huku shukrani zikitolewa kutoka kwa viongozi wa ngazi zote kwa jinsi ambavyo vipindi vya redio hii vinavyoelimisha jamii katika kupambana na ujinga,umaskini na maradhi.

Kwa Neema Fm imeendelea kufanya kazi kwa ubunifu na ufanisi katika vipindi vyake ili kufanikisha maono haya makubwa kwa ajili ya Ufalme wa Mungu.

Fikra Pevu:kipindi chenye mafundisho ya kibiblia, kisaikolojia na uraia ambacho huruka asubuhi baada ya amka uangaze

Yaliyosheheni: ni kipindi chenye kuijuza jamii yale yanayoendelea katika jamii kimatukio,

Full Shangwe ni kipindi burudani za kiufalme ambapo habari zinazohusu muziki wa injili hupatikana hapo  

Kutoka Chumba cha habari ambacho hulenga magazeti na mada mbalimbali pamoja na matukio na Taarifa za habari ambazo zimegawanywa kuhakikisha kila wakati watu wanahabarishwa

Majira ya Ufahamu Na Bishop Augustine Mpemba ambacho huwatoa watu matongotongo ya ufahamu wa neno la Mungu, Msasa wa wiki Kipindi kinachojadili mada za kisisasa, kijamii na kiuchumi.

Fumbua Macho kipindi cha maarifa ya kibishara na ujasiriamali
Vipindi vya Afya Mazingira, wanawake watoto vijana Kona ya Michezo na vingine vingi. 

Timu hii ya watendakazi imeendelea kufanya kazi kwa ubunifu mkubwa ili kuboresha kazi hii na kutimiza malengo ya maono haya ya kiufalme.

Katika muda huu wa miaka 7 Kwa Neema Fm redio imeweza kufanikiwa mengi kama:

Neema Fm kupitia kipindi cha Kwa Neema(kama kilivyojulikana wakati huo sasa kinaitwa Majira Ya Ufahamu)chini ya Mwalim wa Neno la Mungu Bishop Augustine Mpemba akishirikiana na walimu wengine wa Theolojia walijikita katika kufundisha kweli ya Maandiko matakatifu na kufichua fundisho hilo potofu ambalo liliwataka watu kuwa na maji, vitambaa au mafuta ili kupata matokeo ya maombi yao.

No comments:

Powered by Blogger.