MKE AUAWA KWA KUMPUNJA MUMEWE NYAMA
Sababu ya kifo hicho ndiyo inayoonekana kushangaza, kwani inadaiwa kuwa mumewe Nemes Muyombe, alifikia hatua hiyo, baada ya kukasirishwa na kitendo cha kumpunja kitoweo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoani Mbeya Advocate Nyombi, jana alithibitisha kutokea tukio hilo akisisitiza kuwa chanzo cha ugomvi ni kitoweo.
Ilielezwa kwamba, katika tukio hilo, mume alitumia shoka kumkata mkewe na kukimbia huku akiliacha kichwani kwa mkewe.
Kamanda Nyombi alieleza kuwa, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi iliyoko Vwawa wakati uchunguzi na juhudi za kumsaka mtuhumiwa vikiendelea.
No comments: