Header Ads

Breaking News
recent

LOWASSA ATAKIWA NA WANA CCM MBEYA

                     Nape Nnauye akiwa anaongoza maandamano mkoani Mbeya.

                                             Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete.
                                   Edward Lowassa.

WANACHAMA na viongozi wa CCM mkoani Mbeya wamesema wameshangazwa na ziara ya viongozi wao wa kitaifa wanaoongozwa na Katibu wa uenezi wa chama hicho Nape Nnauye kuacha kuwaeleza wananchi jinsi chama hicho kinavyofanya maendeleo kwa ilani ya chama chao badala yake wamekuwa wakijinadi na kuwakashifu kimizengwe waasimu wao kisiasa walioko ndani ya CCM.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mtandao huu baada ya mkutano huo kwisha eneo la Rwanda Nzovwe Jijini Mbeya mwishoni mwa wiki, wafuasi wa chama hicho waliokuwa wametoka katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Mbeya walisema lengo la kundi hilo tayari limejulikana hivyo kuwataadhalisha wanachama wengine kote nchini kutoyumbishwa na kauli za viongozi hao.

Makatibu wa Jumuiya za chama hicho ambao waliomba kutoandikwa majina yao Gazetini walisema kuwa wameshangazwa na viongozi hao kushupalia suala la maamuzi magumu na kupinga wakati ukweli unajulikana.

‘’Kabla hawajafika hapa Mbeya zaidi ya wiki mbili tumekuwa tukifanya vikao vya maandalizi tukitegemea kuwa watakuja kuzungumza vitu vya maana ikiwemo utekelezaji wa ilani ya CCM lakini badala yake wameg’ag’ania kujitaja majina na kujiuza kwa ajili ya uchaguzi ujao’’ walisema makatibu hao.

Nao baadhi ya wajumbe waliokuwa wamehudhuria mkutano huo walisema kuwa mbinu inayotumika na kundi hilo ambalo limeshindwa kujibu hoja ya usaliti wa chama hicho na kuunda CCJ ni mbinu hasi ambayo haitazaa matunda kama wanavyofikiri.
 Mbunge wa Jimbo la Monduli Edward Lowassa na Christopher Sendeka Mbunge wa Jimbo la Simanjiro.
 Rais Jakaya Kikwete kushoto akiwa na Edward Lowassa (Urafiki wa mashaka)
 Nape Nnauye akiwa anahutubia Mkutano wa hadhara Mbeya.

Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani mkoani hapa wamesema waasisi hao wa CCJ wanatumika vibaya na wanaendekleo kujishushia hadhi kwa jamii ambapo juzi Jumapili walipata joto ya jiwe kwa kuzomewa wilayani Kyela.

Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Mbeya John Mwambigija aliliambia Tanzania Daima kuwa CCM imekosa wasemaji ndiyo maana imeamua kuwatuma katika mikoa yote wanachama wa CCJ walioko ndani ya CCM ili kukimaliza chama hicho.

‘’Nadhani kwa kukosa hoja na upako wa kisiasa ndani ya CCM ndiyo maana chama hicho kimeamua kuwatuma hawa CCJ ili waendelee kujiimarisha kwa ajili ya kusajili chama kingine na kuwania urais mwaka 2015’’ alisema Mwambigija.

Naye Katibu wa Chadema mkoa wa Mbeya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mwishoni mwa wiki alisema chama chake kitaendelea kendesha oparesheni ya kuwang’oa Dr.Harrison Mwakyembe na wenzake hivyo mkakati wa CCM wa kuwauza viongozi hao ambao jamiii imewachoka haukitishi chama hicho.


Akizungumza katika mkutano uliolenga ufafanuzi wa kauli mbiu ya kujivua Gamba, Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Taiffa Nape Moses Nnauye alisema kauli mbiu hiyo ina maana nzuru na kwamba CCM tayari imeongeza sumu kwa ajili ya kuwafichua na kuwatosa wale wote wanaoonekana kikwazo katika chama chao na Serikali.

 Edward Lowassa akikagua gwaride la heshima nje ya Tanzania.
 Mbunge wa Jimbo la Kyela Dr. Harrison Mwakyembe akihutubia mkutano Mbeya mjini juzi.

’Ndugu zangu Nyoka akijivua gamba ni kweli sumu huongezeka lakini pia ngozi yake huwa nyororo na anaweza kukimbia vizuri na sumu ambayo imeongezeaka CCM ni kuwabaini na kuwaondoa waovu wote ndani ya chama na Serikali kwasababu watendaji wa Serikali ni wauza duka linalomilikiwa na CCM’’ alisema Nape.
Aidha, alikemea tabia za wauguzi wanaowatukana akina mama wajawazito wanapoenda kujifungua kwa kuwatamkia maneno ya kejeri, Polisi wanaogeuza matatizo ya wanaopelekwa vituoni kuwa biashara kwao na maofisa watendaji wa Vijiji na kata wanaotaka fedha wakati wa kusaini fomu za dhamana na nyaraka mbalimbali zikiwemo zile za mikopo ya vyuo vikuu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti uwanjani hapo Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa na Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sita,Christopha Ole Sendeka mbunge wa jimbo la Simanjiro pamoja na Dr.Harrison Mwakyembe mbunge na Naibu Waziri wa Ujenzi na Miundombinu walisema kuwa azma yao ya kupambana na mafisaji bado ipo pale pale.

Dr. Mwakyembe alisema kuwa wananchi hasa wanachama wa CCM wanapaswa kuwapuuza wale wote wanaosema kuwa Serikali imeshindwa kuchukua maamuzi magumu na kwamba maamuzi magumu yanaweza kufanywa na watu wasiokuwa na hekima wakiwemo vibaka na Majambazi.

‘’Maamuzi magumu yanafanywa hata na vibaka lakini Serikali ya awamu ya Nne inafanya maamuzi Sahihi na makini’’ alisema Dr. Mwakyembe huku akitafsiliwa kuwa ni majibu dhidi ya Mbunge wa Jimbo l Monduli Edwar Lowasa ambaye hivi karibuni amenukuliwa akisema kuwa Serikali iliyopo madarakani inaumwa ugonjwa wa kutochukua maamuzi magumu.

Kwa upande wake Mbunge Samwel Sitta aliongeza kuwa hawatanyamaza kamwe hadi pale watakapo hakikisha dhana ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Jakaya Kikwete  ya ‘kujivua gamba’ inakamilika kwa wale wote ambao hawako safi ndani ya chama hicho kwa kuachia madaraka waliyonayo ndani ya chama na Serikali kwa manufaa ya chama na wananchi kwa ujumla, huku akisahau kuwa aliwahi kumkejeli Rais Kikwete na kumwambia kuwa anapaswa kuongeza ukali kidogo katika maamuzi yake.

“Wakati tunapiga kelele bungeni kuhusu mafisadi mimi na wenzangu,baadhi ya wenzetu walituchukia sana na kujenga chuki dhidi yetu kiasi cha wengine kutaka kuninyang’anya kadi ya chama lakini nilisimama imara na leo tunayaona matunda” alisema Sita.
                        Samwel Sitta kushoto akiwa na Edward Lowassa wakijadili jambo.

Alisema kuwa, Rais alipoona baadhi ya viongozi wanaenda  kinyume na matakwa ya waasisi wa chama hicho,ndipo alipoamua kuanzisha dhana hii ili kurudisha sura nzima ya CCM ya zamani ambayo ilikuwa ikiwajali wakulima na wafanyakazi masikini,hivyo tuna kila sababu ya kutembea kifua mbele katika kulisimamia hili.

Mkutano huo ulihudhuriwa pia na Wabunge wa CCM mkoani hapa, Wenyeviti, makatibu na wajumbe wa ngazi zote kutoka matawi na Kata zote pamoja na wilaya  zinazounda mkoa wa Mbeya ambapo jumla ya wanachama  497 wamepokelewa na kurudisha kadi huku wanachama wapya 2689 wakijiunga na chama hicho na wengine 300 kutoka vyuo vikuu vilivyopo mkoani hapa wakijiunga na chama hicho.

No comments:

Powered by Blogger.