Header Ads

Breaking News
recent

                                         George Mtemahanji kulia akiwa na Shaffih Dauda
Kocha wa Timu ya taifa ya Vijana chini ya Umri wa miaka 23 Jamhuli Kihwelo ametangaza kikosi cha wachezaji 20 kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Visiwa vya Shelisheli

Mechi hizo mbili zitachezwa Julai 27 na 30 mwaka huu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.


Kwa Mujibu wa Julio kikosi hicho kina mabadiliko kadhaa ya wachezaji ambapo safari hii pia wamemwongeza Mchezaji George Mtemahanji ambaye anacheza soka la kulipwa nchini Italia kwenye Seria B katika klabu ya Modena FC.


Mtemahanji amepewa nafasi na kocha Julio ili aonyeshe kipaji chake..


                                                           George Mtemahanji.


Wachezaji hao ni Juma Abdul (Mtibwa Sugar), Himid Mao (Azam), Babu Ally (Morani), Shabani Kado (Yanga), Salum Abubakar (Azam), Godfrey Wambura (Simba), Jabir Aziz (Azam), Seif Juma (Ilala), Khamis Mcha (Azam), Shomari Kapombe (Simba), Jackson Wandwi (Azam).

Wengine ni Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Thomas Ulimwengu (Hamburg SV Ujerumani), Hussein Javu (Mtibwa Sugar), Mohamed Soud (Toto Africans), Jamal Mnyate (Azam), Awadh Juma (Moro United), Salum Kanoni (Simba), Salum Telela (Yanga), Samuel Ngasa (African Lyon) na George Mtemahanji (Modena FC, Italia).

No comments:

Powered by Blogger.