Header Ads

Breaking News
recent

SITTA:- WAPINZANI NI WANAFIKI


  SITTA:- WAPINZANI NI WANAFIKI

Na: Seif Omary
KAIMU KIONGOZI WA SHUGHULI ZA SERIKALI BUNGENI MHESHIMIWA SAMWEL SITTA AMEWATAKA WABUNGE WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM KUTOUMIZWA VICHWA NA WABUNGE WAUPINZANI WANAPOIKOSOA SERIKALI KWA KUWA NI JUKUMU LAO

MHESHIMIWA SITTA AMBAYE PIA NI WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI AMETOA KAULI HIYO LEO BUNGENI MJINI DODOMA WAKATI WA MJADALA WA HOTUBA YA BAJETI YA OFISI YA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

AMESEMA KUWA WAPINZANI WAMEKUWA NA KAWAIDA YA KUKOSOA HATA AMBAPO SERIKALI YA CCM INAPASWA KUPONGEZWA NA KWAMBA KAULI ZAO NI NYEPESI AM,BAZO PIA AMEZIITA BAADHI YA KAULI KUWA NI ZA KINAFIKI

KAULI HIYO AMEITOA BAADA YA MBUNGE WA NZEGA MHESHIMIWA HAMISI KIGWANGALA KUOMBA MWONGOZO WA MWENYEKITI KUFUATIA MANENO YA MBUNGE WA KIGOMA KUSINI MHESHIMIWA KAFULILA ALIYESEMA KUWA SERIKALI YA CCM NI LEGELEGE NA IMESHINDWA KUKUSANYA KODI

AKITOA MWONGOZO MWENYEKITI WA BUNGE MHESHIMIWA JENISTER MHAGAMA AMEMTAKA MHESHIMIWA KAFULILA AFUTE KAULI YAKE ALIYODAI KUWA NI YAMAUDHI KWA MUJIBU WA VIFUNGU

MHESHIMIWA KAFULILA AKAGOMA KUFUTA KAULI HIYO HUKU AKISISITIZA KUWA AMENUKUU MANENO YA MWALIMU NYERERE HIVYO ALIKUWA SAHIHI NA KISHA KUFUATIWA NA ZOGO KUTOKA KWA WABUNGE AMBAPO WALE WA CHAMA TAWALA WALITAKA AFUTE KAULI HIYO HUKU WAPINZANI WAKISEMA KUWA KAULI HAIWEZI KUFUTWA KWA KUWA NI NUKUU YA MWALIMU NYERERE

AKIHITIMISHA KUHUSU MWONGOZO MWENYEKITI WA BUNGE AMETAKA KAULI THABITI NA ZENYE HEKIMA ZA HAYATI BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE ZITUMIKE IPASAVYO NA ZIENZIWE KWA UMAKINI KWA MASLAHI YA BUNGE LA WATANZANIA KWA UJUMLA BILA KUPOTOSHWA

HATA HIVYO MWENYEKITI HUYO WA BUNGE ALIKATAA MIONGOZO NA TAARIFA ZA WABUNGE KADHAA AKIWEMO MHESHIMIWA ZITTO KABWE KWA KUWA MUDA ULIKUWA UMEKWISHA HALI ILIYOONGEZA ZOGO NA KELELE KUTOKA KWA WABUNGE

No comments:

Powered by Blogger.