Header Ads

Breaking News
recent
UNHCR YAONYA DHIDI YA WAKIMBIZI SOMALI
Watu wengi, wakiwemo watoto, wanakufa wakiwa wanaukimbia ukame mkubwa huko Somalia.

Shirika la Umoja wa Mataifa  la kuwahudumia wakimbizi, UNHCR, lilionya leo kwamba juhudi ziko hatarini ya kuzidiwa na idadi kubwa ya wakimbizi wanaowasili katika makambi.

Msemaji wa UNHCR,  Melissa Fleming aMEsema watu wengi wanakufa njiani.


Hajaweza kutoa idadi ya vifo hivyo lakini alisema kuna hadithi za kutisha kutoka kwa akina mama waliopoteza watoto wao wakiwa njiani, na wengine ambao wamelazimika kuwaacha nyuma watu kutoka familia zao ambao ni wagonjwa.

Wasomali 1,700 wanawasili kila siku katika kambi ya Dollo Ado, kusini mashariki ya Ethiopia, wakitafuta vyakula na maji, na katika nchi jirani ya Kenya, kila siku wanawasili watu 1,400 katika kambi ya Daddab iliyosheheni wakimbizi.

Bibi Melissa Fleming amesema mifumo ya kukabiliana na mahitaji ya vyakula na huduma za afya kwa ajili ya wakimbizi inapindika.

No comments:

Powered by Blogger.