Header Ads

Breaking News
recent

YANGA YAIFUATA SIMBA KOMBE LA KAGAME

FUATILIA MOJA KWA MOJA MECHI YA FAINALI KESHO JUMAPILI KUPITIA MTANDAO HUU www.msasawawiki.blogspot.com

Baada ya Simba ya Dar es Salaam, kufanikiwa kufika katika hatua ya fainali ya Kombe la Kagame kwenye michuano hiyo inayoendelea jijini Dar, baada ya kuwaondosha El-Mereikh ya Sudan juzi kwa mikwaju ya penati kufuatia kumalizika kwa dakika 90 huku timu hizo zikiwa sare ya 1-1. Jana tena ndani ya muda kama wa juzi hatua za mikwaju ya penati hatimaye mtani wake wa Jadi Yanga ambaye alikutana na timu ya St. George ya Ethiopia wamefanikiwa nao kutinga fainali kwa style hiyohiyo katika mchezo wao wa nusu fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa kwa kushinda penati 5-4. Ndani ya dakika 120 timu hizo zilitoka 0-0.

Fainali inayokutanisha watani hao itakuwa siku ya Jumapili ya tarehe 10 july, ambapo kabla jumamosi mchezo kati ya St. George v/s El-Mereikh utapigwa kumtafuta mshindi wa tatu.

No comments:

Powered by Blogger.