HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA JUMAPILI NDANI YA NYUMBANI HOTEL
Classic Gospel Concert NDANI YA Mwanza
Kuna matamasha mengi yanafanyika lakini hili Mungu alijidhihirisha kwa namna ya tofauti na kugusa mioyo ya Wengi. Hakukua na Intertaiment na kwa mara ya kwanza kumeshuhudia watu wakisimama kwa muda mwingi wa concert wakimwabudu Mungu na sio kukaa na kuwashangaa waimbaji walioko Madhabahuni.
HAPA Adolf Nzwalla Akimsifu MUNGU |
Taratibu tunahama katika level za kushabikia Burudani za Injili tunaenda kwenye level za kuabudu ambazo zinaugusa moyo wa Mungu. Na kwa wanaofatilia watagundua kwa sasa nchi nzima Matamasha yanafanyika. Arusha wako HOT, Mwanza, Mbeya, Morogoro Dar ndio usiseme hapo utaona pamoja na mapungufu yaliyopo taratibu uchaji halisi unaiteka nchi.
Concert zinafanyika na watu wengi wanahudhuria pasipo uwepo wa Rose Mhando, Shusho, Nkone wala Prominent figure yeyote. Na hii sio kwa Corncerts tu bali hata makanisani uchaji wa Mungu kupitia sifa na kuabudu unazidi kuimarika siku hadi siku.
Concert zinafanyika na watu wengi wanahudhuria pasipo uwepo wa Rose Mhando, Shusho, Nkone wala Prominent figure yeyote. Na hii sio kwa Corncerts tu bali hata makanisani uchaji wa Mungu kupitia sifa na kuabudu unazidi kuimarika siku hadi siku.
Hosanna Praise Team wakiimba
Kuna wengi wanasema Kanisa la Tanzania limejaa migogoro baina ya kanisa na kanisa, watumishi kwa watumishi, watumishi na waimbaji wameweka maslahi yao binafsi mbele kuliko Ufalme wa Mungu mi nasema FINE wakiri wanavyokiri ila nikionacho mimi ni kuwa Mungu yuko Karakana{Workshop} akjiandalia jeshi lake kwa utukufu wake ambalo kamwe halitopiga MAGOTI kwa Baali.
Micc Praise Team wakiwa Jukwaani
No comments: