Header Ads

Breaking News
recent

JAMII YATAKIWA KUTOWAACHA WATOTO YATIMA

JAMII YATAKIWA KUTOWAACHA WATOTO YATIMA


Gladness Mushi wa Fullshangwe-Arusha
JAMII nchini imeaswa kuwajali watoto waishio katika mazingira magumu na wale walioko kwenye vituo vya kulelea watoto yatima kwa kuwapatia msaada mbalimbali na kuondokana na tabia ya kuwanyanyapaa na kuwaona ni mzigo kwa jamii.
Kadhalika watoto waishio na virusi vya ukimwi kwa kuwapatia ushirikiano wa kutosha ikiwa ni pamoja na kuwajali kwa kuwapa huduma mbalimbali zinazostahili kwa kuwa hata wao wana haki ya kuishi kama watoto wengine.
Rai hiyo,imetolewa mwishoni mwa wiki na meneja wa mamlaka ya mawasiliano kanda ya kaskazini (TCRA),Annette Matindi wakati alipokuwa akikabidhi zawadi mbalimbali vikiwemo vyakula na mashuka kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Matonyok kilichopo Olasiti jijini Arusha.
Hafla hiyo ililenga kuuaga mwaka 2011 na kuukaribisha mwaka 2011 iliyofanyika katika viwanja vya General Tyre jijini Arusha.
Matindi alisema kuwa jamii inapaswa kujitolea kwa faida kidogo inayopata kwa kuyapatia msaada makundi yasio na uwezo wa kujitegemea hususani watoto yatima ambao hawana wazazi na wanaishi kwa kutegemea misaada ya wahisani ,wafadhili na wasamalia wema.
Alisema hakuna haja ya kuwanyanyapaa watoto hao kwa vile wengi wa watoto hao wanatoka mwiongoni mwa jamii kutokana na mifarakano mbalimbali ya wanandoa ama familia na kupelekea watoto hao kushindwa kuishi na wazazi waona kujikuta wakikimbilia mitaani.
Alisema TCRA imeamua kutumia siku ya familia sanjari na kuuaga mwaka 2011 na kuukaribisha mwaka 2012kula chakula na watoto hao baada ya kutambua umuhimu wao.
Kwa upande wa mlezi wa kituo hicho, bi Emmy Silayo pamoja na kushukuru kwa msaada huyo alisema ipo haja kwa kila jamii kuiga mfano huo kwa kujitolea walau kidogo kwa kusaidia vituo vya kulelea watoto yatima. Alisema kituo hicho kina zaidi ya watoto 40 ambao ni kuanzia umri mwaka mmoja hadi 18 na kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa chakula na shule ya kuwafundishia watoto hao. Alisema kwa sasa kituo hicho kinategemea zaidi kuomba misaada kutoka mashirika mbalimbali na watu binafsi hivyo aliiomba jamii kuguswa na msaada huo uliotolewa na TCRA na kuona umuhimuwa wao kuwasaidia watoto hao

No comments:

Powered by Blogger.