WANACHAMA WAILILIA TIMU YA AFC ARUSHA KUSHUKA DARAJA.
Wanachama na wananchi wa mkoa wa Arusha wamepokea kwa masikitiko makubwa kitendo cha timu yao kushuka daraja kutokana na malumbano ya viongozi yaliyopo.
Wanachama hao ambao wameomba hifadhi ya majina yao walitoa malalamiko yao wakiwa na uchungu mkubwa kwani kutokana na kushuka daraja kwa timu yao.
Walisema kuwa wanaitupia lawama kubwa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Arusha kwani ndicho kilichofanya hadi timu yao ikashuka.
"uanajua tunalalamika kwanini tuliwaambia hawa viongozi wa wilaya watupe timu yetu kama ikifa ifie mikoni mwetu wakagoma sasa wanaona walichokuwa wanakita ka wamesababisha hadi timu yetu ikiashuka daraja "alisema mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Hassani.
Nipashe lilizungumza na baadhi ya wapenzi wa soka wa mkoa wa Arusha nao walisema kuwa wamesikitishwa sana na kitendo cha timu hii kushuka daraja kwani kwani walikuwa wanaitegemea kama ndio timu ya wananchi.
"kwakweli tunasikitishwa sana kwa kitendo cha timu hiikushuka daraja kwani ndiho timu tulikuwa tunaitegemea katika soka la mkoa wa Arusha sasa watu wacheche wamesababisha hata timu yetu ikashuka tunalaani sana.
Nipashe haikuishia hapo bali lilizungumza na mmoja wa waandishi wa habari Mahmoud Ahmad alisema kuwa amesikitishwa sana kuona timu ambayo ilikuwa ndio kioo cha michezo katika mkoa wa Arusha ikiachwa yatima hadi kufikia kushuka daraja.
alitoa ushauri kwa viongozi wa mkoa kuandaa timu mapema na kutafuta wafadhili kwani wameona mechi tatu za timu ya Jkt Oljoro zikipotea kitu ambacho sio jambo zuri na inaashirika kuporomoka kwa soka mkoani Arusha.
"viongozi wasipoangalia kwa umakini tutabaki kuwa wasindikizaji katika soka hapa nchini kitu ambacho ni aibu kubwa sana kwani awali katika mpira wa mkoa huu kulikuwa na soka la zuri ambalolilimsisi mua kila mmoja lakini kwa sasa limeondoka hamna soka kabisa tunaelekea kuwa watazamaji wa timu zingine tu " alisema Mahamoud
Aidha alitoa wito kwa viongozi ambao lawama kubwa zimetupiwa kwao kuwa wajirekebishwe na watafute kazi zakufanya na sio kutegemea mpira jambo ambalo linawafanya wakae kupigiana fitina katika soka na sio kusaidia soka la mkoa wa Arusha
Kwa upande wake katibu wa soka wa wilaya ya Arusha Zakayo Mjema alisema kuwa yeye amepokea kwa masikitiko makubwa swala hili kwani wao kama chama cha mpira walishirikiana kwa kila njia kuinusuru timu hii lakini walishedwa.
Alisema kuwa walitafuta ushirikiano kutoka kwa wanachama wa AFC lakini hawakupata lakini kwa sasa timu hii imeshuka daraja wanatupiwa lawama kitu ambacho sio cha haki .
Timu hii ya AFC imekuwa ni timu ya kung'ang'aniwa na watu ambao wengi wao wamekuwa wakiifanya timu hii shamba la bii hali iliyofanya kuifikisha timu hii hapa ilipo na katika timu hii wachezaji wenyewe wamefanya kazi ya ziada na kujituma vilivyo kwani kutokana na malumbano ya viongozi hao na wanachama yalipelekea hata wacheza kwenda kucheza mechi bila kula na wengine kuishi hata bila ya kupewa posho za kujikimu.
No comments: