Header Ads

Breaking News
recent

YANGA NA MTIBWA KUUMANA LEO LIGI KUU YA VODACOM 2011/2012



Ligi Kuu ya Vodacom ambayo iko katika raundi ya 16 inaendelea tena leo kwa  kwa mechi moja kati ya Yanga na Mtibwa Sugar. 
Mechi hiyo namba 112 itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni.
Mechi hiyo itachezeshwa na mwamuzi Ibrahim Kidiwa kutoka Tanga wakati wasaidizi wake ni Michael Mkongwa kutoka Iringa na Kudura Omary wa Tanga. Kamishna wa mechi hiyo ni Mohamed Nyange kutoka Dodoma.
   
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 3,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP B na C, na sh. 15,000 kwa VIP A.

No comments:

Powered by Blogger.