Tanzania yapanua wigo wa sensa kukabiliana na umaskini.
Tanzania inapanua wigo wa sensa yake mwaka huu ili kuongeza maswali yanayohusu ulemavu, afya ya akina mama wajawazito na vifo vya watoto wachanga, gazeti la The Citizen la Tanzania liliripoti Jumanne (tarehe 15 Machi). "Kiwango cha vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga kitalinganishwa na viwango vya nchi nyingine," alisema Albina Chuwa, mkurugenzi mkuu wa Idara ya Takwimu ya Taifa yaTanzania akiongeza kwamba mchakato wa sensa utaanza mwezi Agosti.
Alisema madodoso yatakuwa na takriban maswali 61, majibu yake yatabaki kuwa siri. Data zitakazokusanywa kutoka kwa Watanzania takribana milioni 40 zitatumika kutekeleza programu za maendeleo ambazo zinahimiza kukua na kukabiliana na umaskini, Chuwa alisema.
Sensa zitakusanya pia data zinazohusu takwimu za kilimo ikiwa ni pamoja na idadi ya mifugo kwa kila kaya.
No comments: