Header Ads

Breaking News
recent

CHAMA CHA WALEMAVU MWANZA WAIOMBA SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA WALEMAVU.


SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WALEMAVU TANZANIA (SHIVIWATA) MKOA WA MWANZA WAMEIOMBA SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA WALEMAVU KWAAJILI YA KULINDA HAKI NA USALAMA WAO.
 HAYO YAMEBAINISHWA NA KATIBU WA SHIVIWATA MKOA WA MWANZA BI. LUCY MAKUNE WAKATI  AKIZUNGUMZA  NA WANDISHI WA HABARI  OFISINI KWAKE, AMBAPO AMESEMA MIUNDOMBINU MIBOVU NI CHANGAMOTO KWA WALEMAVU HALI INAYOSABABISHA KUTOKUTEKELEZWA KWA  SHUGHULI MBALIMBALI KWAO.



AMEZITAJA ATHARI  ZINAZOTOKANA NA CHANGAMOTO HIYO KUWA NI PAMOJA NA UKOSEFU WA AJIRA,USHIRIKISHWAJI HABA KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO ,UNYANYAPAA UTEGEMEZI NA KUISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU KWA UJUMLA



BI LUCY AMETOA MWITO KWA SERIKALI PAMOJA NA SEKTA BINAFSI  KUTOA MISAADA MBALIMBALI KATIKA VYAMA VYA WALEMAVU ILI KUWAWEZESHA KUJITEGEMEA NA KUJIKWAMUA KIMAISHA



WAKIZUNGUMZA NA KWANEEMA FM BAADHI  YA WALEMAVU WAMEIOMBA JAMII KUBADILI MITAZAMO YAO JUU YA WALEMAVU NA KUWATAKA KUFAHAMU KUWA WATU WOTE NI SAWA HIVYO WASIWATENGE ILA WASHIRIKIANE NAO KATIKA MAMBO MBALIMBALI YA JAMII.

No comments:

Powered by Blogger.