HABARI KWA UFUPI: KIKRISTO KUTOKA KWA NEEMA FM RADIO ILIYOSOMWA SAA 3:00 ASUBUHI 07/10/2013.
MWANZA
kanisa la the Apostolic Church tanzania limemsimika Apostle Posian Martine kuwa kiongozi wa kitaifa wa
kanisa hilo.
Sherehe hizo zilihudhuriwa
na mwakilishi wa Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya ilemela Bw: James Chuwa na
kumkabidhi katiba ya nchi ya Tanzania na kumpatia katiba ya kanisa,
WAKATI HUO
HUO
wakristo wamekumbushwa
kwamba Mungu anafanya kazi na wale wampendao katika kuwapatia mema yote.
hayo yamesemwa na
mchungaji kiongozi wa kanisa la maranatha faith mission asesmblies of God Tanzania Irene george katika ibada ya jumapili ilyofanyika katika kanisa hilo parishi ya
isamilo.
Akisoma neno la Mungu
katika kitabu cha waraka wa Paulo kwa Warumi 8: 26-28 mchungaji Irene amesema Mungu hufanya kazi na wale wampendao katika kuwapatia haja zao.
Mchungaji Irene amesema
wakristo wanatakiwa kuwa watendaji wa neno la Mungu kwa kuwa Mungu huwapa Roho Mtakatifu ambaye huwaombea kila siku.
Amesema Roho Mtakatifu
huwasaidia wakristo katika yote na kuichunguza mioyo ya wakristo ili awatimizie
mahitaji yao.
KIMATAIFA
Kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amelitaka kanisa lake
na waamini kujihusisha moja kwamoja na kutafuta suluhu ya matatizo
yanayoikabili dunia kwa sasa, kama alivyofanya Mtakatifu Francis wa Assisi.Papa Francis ambaye alichukua jina hilo kutokana na kuvutiwa na maisha ya mtakatifu huyo, alitoa wito huo kwenye ibada maalumu ya hija ya watakatifu iliyofanyika kwenye Mji wa Assisi alikozaliwa mtakatifu Fransis.
Alisema umefika wakati kwa Kanisa kugeuka na kurejea misingi yake ya imani inayolenga kujali utu na kusaidia wanyonge na wenye shida, kurejea mahitaji muhimu ya kiimani kama alivyofanya mtakatifu huyo.
Papa huyo kutoka Argentina pia alitoa salamu zake za rambirambi kutokana na ajali ya meli iliyowakumba wahamiaji kwenye Kisiwa cha Lampedusa huko Italia na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 111 na wengine wengi wakiwa hawajulikani walipo.
Alisema anashangazwa na namna dunia isivyojali kuhusu mamilioni ya watu wanaokimbia utumwa, njaa na kukimbia maeneo yao kwa ajili ya kutafuta uhuru na namna wengi wanavyokufa kama ilivyotokea kwenye ajali hiyo ya juzi na kusababisha vilio kwa maelfu leo.
Tunahitaji kuthamini kilio cha wale wanaobubujikwa na machozi, wanaotaabika au kufa kwa sababu ya machafuko, ugaidi, uharamia au vita kwenye ardhi takatifu aliyoithamini Mtakatifu Francis, huko Syria, Mashariki ya Kati na maeneo yote duniani," alisema Papa Francis.
Ziara hiyo ya Francis kwenye Mji wa Assisi inajenga dhana
tofauti na waliomtangulia, John Paul II na Benedict XVI kwa kuwa amelenga kutoa
ujumbe wa kitume kuhusu kuwajali masikini zaidi ya ujumbe wa kuhamasisha
ushirikiano na mwingiliano.
Mhariri Mkuu:Jeston Kihwelo
Simu:0768-248864.
Mhariri Michezo:Erasto Juma
Simu:0767-200986.
No comments: