kwa neema fm radio 98.2MHz tunaangaza
|
Askofu Mkuu wa makanisa ya Tanzania Field of Evangelism (TFE) Na Mmiliki wa kituo cha Redio ya Kwa Neema jijini Mwanza,Dr:Bishop Augustine Mpemba.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Hivi
karibuni baadhi ya vyombo vya habari vimetoa habari ambazo ndani yake zimemtaja
Askofu Mkuu wa Makanisa ya TFE Dr. Bishop Augustine Mpemba kuwa yuko
“MAFICHONI” na anatafutwa na Serikali ya Tanzania kwa kuwa alitoa CDs au DVDs
za uchochezi.
Tunapenda
kuchukua nafasi hii kutoa ufafanuzi kuwa Kiongozi wa Makanisa ya TFE Bishop Dr.
Augustine Mpemba hayuko “MAFICHONI”, hajawahi kutoa CD au DVD za uchochezi na
hatafutwi na Serikali ya Tanzania.
Wakati
akihojiwa na Mhariri wa Gazeti la SAUTI YA AFRIKA mapema mwaka 2013, Bishop Dr.
Augustine Mpemba alieleza kwa kina jinsi alivyoandika barua pepe kwa Waziri wa
Mambo ya Ndani wa wakati ule Dr. Emmanuel Nchimbi na nakala yake kupatiwa
Kamanda wa Polisi wa Mkoa Mwanza wa kipindi kile ambaye sasa ni IGP. Katika
barua pepe hiyo alielezea yuko nchini Marekani, anafanya nini na ni lini
atarudi nchini (Ufafanuzi huu pia aliutoka katika mahojiano na Gazeti la
Mtanzania Mwezi Julai mwaka 2014).
Kwahiyo
Serikali haiwezi kuwa ina mtafuta mtu inaye jua mahali alipo na ina uwezo
mkubwa wa kumpata ikitaka kufanya hivyo. Kwa ufafanuzi Zaidi pia ni kuwa
Taifa kubwa la Marekani linaloheshimika duniani kwa demokrasia na haki sio
mafichoni.
Kuhusu CD
au DVD za uchochezi; si kweli kuwa Bishop Dr. Augustine Mpemba alitoa DVD yenye
somo lenye kichwa cha 'Inuka Chinja Ule'. Jambo hili wakati mwingine tumekuwa
tukisikia likisemwa katika Magazeti na viongozi wa Jeshi la Polisi. Hii peke
yake ilitupa picha kujua kuwa hawakukiona walichokuwa wakikitangaza.
Ukweli wa
kilichotolewa na kwa nini ili yamkini umma wa wapenda haki wajue kwa ufasaha
(ufafanuzi huu pia ulitolewa kwenye ukurasa mzima wa Gazeti la Mtanzania mwezi
Julai mwaka 2014):
Tarehe 6
Feb 2013, Maaskofu wa Jijini Mwanza kutoka Taasisi za TEC, CPCT na CCT walikutana
na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mwanza ili kumwelezea kutokuridhika kwao na kauli za
kiongozi wa Mkoa kuhusiana na jambo hili la kuchinja.
Katika
kikao hicho ndipo Mwenyekiti huyo kwa nia njema akawaomba Maaskofu wamwandalie
mafundisho hayo ili ayawakilishe kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa ajili ya
kutafuta ufumbuzi. Maaskofu waliokuwepo wakapendekeza wanazuoni watano ili
kuandaa mafundisho ya kibiblia kuhusiana na somo hili.
Askofu Augustine Mpemba
alikuwa mmoja katika wanazuoni waliopendekezwa na kupitishwa.
Tarehe 8
Feb 2013 wanazuoni hao walikutana na baada ya tathmini ya kibiblia wakarekodi
audio CD ya INUKA, CHINJA, ULE (SIYO DVD). Tunasisitiza tena kuwa
walirekodi audio CD ya INUKA, CHINJA, ULE.
Tarehe 13
February 2013 waliisambaza CD hiyo kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa, pia alipatiwa
Mkuu wa Mkoa Mwanza na Wakuu wa Wilaya za Ilemela na Nyamagana. Walifanya hivyo
kwa sababu katika kikao chao na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mwanza ilionekana
kuwa uelewa huo wa kuchinja kwa mujibu wa Biblia haukuwemo ndani ya viongozi
wengi.
Cha ajabu
na kushangaza sana ni kwamba CD hiyo ambayo ilisambazwa kwa mara ya kwanza
tarehe 13 February 2013 kwa viongozi tu ndiyo ikataka kulazimishwa ili ionekane
kuwa ndiyo iliyosababisha mauaji ya Mchungaji Mathayo Kachili yaliyotokea
tarehe 11 February 2013. Mkakati ulikuwa ni kumhusisha Askofu Augustine Mpemba
na mauaji ya Mchungaji Kachili.
Kama CD
ndiyo ingekuwa ni sababu ya unao daiwa kuwa ni uchochezi na hivyo kufunguliwa kesi,
basi kesi hiyo ingewahusu Wachungaji watano ambao walirekodi CD hiyo.
Hatujapata taarifa yeyote toka kwa Wachungaji wenzake kuwa kuna kesi
imefunguliwa na Serikali dhidi yao au dhidi ya Askofu Mpemba tangu wakati huo.
Tuna amini kuwa huo ni uzushi wa kuipaka matope Serikali yetu.
Kuhusu
habari kuwa Bishop Dr. Augustine Mpemba alitumia njia ya Video wakati wa
uzinduzi wa Vitabu vyake vya Kulipenda Taifa na Kulijenga na Mawazo ya
Mabilionea mwezi Aprili Mwaka 2015; hiyo ni teknolojia ya kawaida inayotumiwa
hata na marais na viongozi wa umoja wa mataifa katika mikutano mbalimbali
duniani kwahiyo isichukuliwe kuwa ni hoja ya “KUJIFICHA”.
Tunasisitiza
kuwa Askofu Mkuu wa Makanisa ya TFE Bishop Dr. Augustine Mpemba yuko nchini
Marekani kwa masomo na kazi ya umisionari, hatafutwi na serikali ya Tanzania na
kwamba hakusambaza CD au DVD za uchocheza mahali popote.
Amani ya
Mungu iendelee kuwa nasi daima.
KATIBU MKUU,
TANZANIA FIELD EVANGALISM (TFE) CHURCHES.
29 APRIL
2015
|
No comments: