SOMA TAARIFA YA JESHI LA POLISI JUU YA UGAIDI,ISOME HAPA
kwa neema fm radio 98.2MHz tunaangaza
Katika siku za hivi karibuni kumeibuka
tabia ya baadhi ya watu wachache wasiofahamika kutunga na kusambaza ujumbe
kupitia simu za mikononi na mitandao mbalimbali ya kijamii wenye lengo la
kuwatia hofu wananchi, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Aidha, watu hao wanaosambaza taarifa hizo wanajifanya kwamba taarifa hizo zimetoka kwenye taasisi za kimataifa na taasisi zingine zinazoaminika jambo ambalo siyo kweli.
Aidha, watu hao wanaosambaza taarifa hizo wanajifanya kwamba taarifa hizo zimetoka kwenye taasisi za kimataifa na taasisi zingine zinazoaminika jambo ambalo siyo kweli.
Jeshi la Polisi nchini linawataka wote
wenye tabia hiyo kuacha mara moja na badala yake, endapo mtu yeyote anayo
taarifa ya uhalifu wa aina yoyote ama kikundi chochote cha uhalifu atoe taarifa
hiyo katika kituo chochote cha Polisi au kupitia simu za makamanda wa polisi wa
mikoa ama vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili taarifa hizo ziweze
kufanyiwa kazi haraka.
Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea na
uchunguzi wa taarifa zote zinazopokelewa ili kuhakikisha kwamba usalama wa raia
na mali zao unaendelea kuimarika.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kusambaza ujumbe wenye mlengo wa upotoshaji, uchochezi ama kuwatia hofu wananchi.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kusambaza ujumbe wenye mlengo wa upotoshaji, uchochezi ama kuwatia hofu wananchi.
Imetolewa na:-
Advera Bulimba -SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
WEKA MAONI YAKO HAPA
No comments: