Corinthians yaongeza dau kwa TEVES
Klabu ya soka ya nchini Brazil, Corinthians, imeongeza pesa itakazotoa katika juhudi za kumsajili nahodha wa Manchester City, Carlos Tevez.
"Ninafahamu wameongeza pesa", wakala wa Tevez, Kia Joorabchian aliielezea BBC, "lakini ombi hilo liliwasilishwa Ijumaa, na hizi ni hatua za mwanzo tu."
Hawataki kuharakishwa kuafikia makubaliano upesi, lakini meneja Roberto Mancini atapata nafasi bora zaidi katika kumtafuta mchezaji wa Atletico Madrid ya Uhispania, Sergio Aguero.
City wanahisi hawajapungukiwa kifedha, na kwa hiyo hawana shinikizo katika kumuuza Tevez, ambaye pia ana mkataba mrefu, na inaaminika ni zaidi ya pauni lakini mbili kwa wiki.
Kwa hiyo ahadi za Corinthians huenda zikakosa kuivutia Manchester City katika kumuuza Tevez, mwenye umri wa miaka 27, na aliyeisaidia klabu katika kulipata kombe la FA, na timu kufuzu kuingia ligi ya klabu bingwa barani Ulaya.
Kuhamia Marekani Kusini ni jambo ambalo litamsaidia Tevez katika kuikaribia zaidi familia yake.
Iwapo ataondoka, raia mwenzake wa Argentina, Aguero, na mwenye umri wa miaka 23, na ambaye huichezea Atletico, anatazamiwa kujaza pengo litakaloachwa na Tevez.
Lakini City hawataki kufanya juhudi hizo kabla ya kuwa na uhakika ikiwa Tevez ataondoka au la.
No comments: