HAMMAM AWAPUUZA WAPELELEZI WAKE
Shirikisho linalotawala mchezo wa Kandanda Duniani FIFA linasema kuwa Mwanachama wake Mohamed Bin Hammam amekataa kuzungumza na wakuu wake waliotumwa kupeleleza madai kuwa alijaribu kuwahonga wakuu wa vyama vya mpira vya kanda ya Caribbean.
Taarifa iliyochapishwa na kundi lijulikanalo kama Freeh Group International, shirika huru la upelelezi linalomilikiwa na aliyekuwa mkuu wa FBI hapo zamani limehitimisha taarifa yake kwa kusema kuwa ''Hakuna ushahidi bayana unaomhusisha Bw.Hamam na jaribio la kutoa hongo moja kwa moja au malipo taslimu, kilichopo ni ushahidi wa dhana, kuwa raia huyo wa Qatari ndiye aliyetoa pesa hizo.
Ripoti ya Freeh iliyotolewa na wakili wa Bw.Hamam kwa vyombo vya habari imesema kuwa Bw.Hamam amekataa kuzungumza na wanaoendesha upelelezi huo ingawa amesema atakua tayari kuzungumza mbele Kamati ya maadili ya FIFA.
Mashirika saba kutoka kanda ya Caribbean yamewambia wapelelezi kuwa walipewa au walikubali zawadi za hadi dola za kimarekani 40,000 wakiwa kwenye chumba kimoja cha Hoteli ya Hyatt Regency mnamo tareh 10 mwezi May baada ya hotuba ya Bw.Hammam akijieleza katika kampeni za uchaguzi wa Rais wa FIFA.
Jack Warner hata hivyo, hatotakiwa kufika mbele ya Kamati ya maadili kutokana na kwamba FIFA ilimuondolea tuhuma zote baada ya uwamuzi wake wa kujiuzulu kutoka shughuli zote za FIFA.
No comments: