Man City yakubali kumuuza Tevez
Meneja wa klabu ya Manchester City, Roberto Mancini, amesema makubaliano yameafikiwa na klabu ya Corinthians ya Brazil, kumhusu mshambulizi kutoka Argentina, Carlos Tevez.
Wiki iliyopita, ahadi za Corinthians kumnunua kwa pauni milioni 39 zilitupiliwa mbali na City, na inaaminika klabu kinataka kumuuza kwa pauni milioni 50."Tuna makubaliano na Corinthians, lakini Carlos bado ni mchezaji wa City", Mancini alilielezea alipozungumza katika matangazo ya televisheni ya Sky Sports.
Klabu hiyo ya Sao Paulo, nchini Brazil, na huku ikiwa ndio tu imefanya makubaliano ya kupata fedha zaidi kutoka televisheni, ina juhudi za kumsajili Tevez na kumrudisha katika klabu ambayo aliweza kusifika kama mchezaji mahiri, na akipata ufanisi mkubwa.
Kurudi Marekani ya Kusini pia kutamsaidia Tevez kuwakaribia watoto wake wawili.
No comments: