Header Ads

Breaking News
recent

WIZI WA KUTUMIA MITANDAO YA SIMU WAWAINGIZA MJINI WAFANYABIASHARA MBEYA



                                  Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi.

KUNDI la wezi wa kimataifa wanaotumia njia ya wizi wa kieletroniki kupitia mitandao ya simu za mkononi wametua mkoani Mbeya na kufanikiwa kuwaibia baadhi ya wafanyabiashara mamilioni ya fedha.

Mbinu zinazotumiwa na wezi hao zimekuwa zikiambatana na vitisho vikali dhidiya wafanyabiashara waliolengwa na kundi hilo,wengi miongoni mwao wakiwa ni wamiliki wa hoteli za kisasa jijini Mbeya na wilayani kupitia Umoja wa wamiliki wa hoteli mkoa wa Mbeya(UWAHOMBE).

Nyendo za wafanyabiashara waliopokea vitisho na wengine wakiwa tayari wameibiwa fedha nyingi huku wakisita kutaja kiasi walichoibiwa kupitia njia ya mawasiliano ya fedha ya M-Pesa kutoka Kampuni ya Vodacom.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya ,Advocate Nyombi alipopigiwa simu kuzungumzia aina mpya ya wizi huo,alisema kuwa hana taarifa na kuahidi kutoa ushirikiano jioni ya siku hiyo kwa kuwa alidai yupo wilayani Kyela kikazi.

“Sina taarifa kama kuna wafanyabiashara wameibiwa na wala sijui kama wizi huo upo,mimi nipo Kyela kikazi jioni nitakaporudi nitakupigia naomba usubiri nirudi kwani wangekuwa wametishiwa wangeripoti sina habari” alisema Kamanda Nyombi ambaye hakuweza kutekeleza ahadi ya kutoa taarifa  kama alivyoahidi.

Wafanyabiashara wamekuwa  wakihaha nje ya kituo cha kati cha polisi jijini Mbeya huku wakijieleza kuwa wamefika hapo ili kutoa taarifa za vitisho kutoka kwa watu wasiojulikana ambao wanawalazimisha kutoa fedha.

Hata hivyo taarifa za ndani kutoka kituoni hapo zinadai kuwa mmoja wa wezi hao wanaojihusisha na wizi wa fedha kupitia kwenye mitandao ya simu amekamatwalicha ya jeshila polisi kutokuwa wazi zaidi kuhusu matukio hayo ambayo yanaonekana kuwajengea hofu kubwa wafanyabiashara.

Baadhi ya taarifa za vitisho ambazo wafanyabiashara kadhaa wamekuwa wakitumiwa zinasomeka hivi “Ndugu tunakuomba utujulishe kama utatupatia au la ili sisi tujuwe cha kufanya cha kufanya kutoka hivi sasa,japokuwa tulikuwa hatukuhitaji kuleta simanzi Mwambena tuna mitindo kama 6” ilisema sehemu ya ujumbe huo wa meseji.

Nyingine “Boss tunahitaji kiasi cha Sh milioni 5 kuzuia mpango mchafu dhidi yako,mpaka kesho asubuhi uwe umekwisha tuma kwenye M-pesa,ni maharamia wa Afrika mashariki siku njema” ujumbe huu alitumiwa mmoja wa wafanyabiashara jina tunalo.

Mfanyabiashara huyo baada ya kushindwa kutekeleza maagizo hayo chumba kimoja kwenye hoteli yake  kilichomwa moto kisha akapokea ujumbe ufuatao “Haya boss ngumi hiyo tumekupiga mchana ili watu wakusaidie kuzuia hasara,subiri ngumi ya bila msaada nyingine ukizidi kuwa mkaidi” ulisomeka ujumbe huo.

Mwenyekiti wa UWAHOMBE,Jeremiah  Mahenge(Vamponji) alipohojiwa alisema kuwa taarifa za kuwepo kwa matukio hayo zipo na kukiri kuwa tayari mmoja wa watuhumiwa hao amekwisha kamatwa na polisi na ndiye aliyedaiwa kuchoma moto chumba cha hoteli hiyo baada ya mtego wake kunaswa alipokuwa akienda kuchukua fedha za M-pesa Vodacom alizoiba kimtandao.

No comments:

Powered by Blogger.