
CHANCELA wa Ujerumani Angela Merkel anazuru nchi tatu barani Afrika kujadili jinsi ya kuwa na ushirikiano wa kiuchumi hususan sekta ya nishati.Ujumbe wa viongozi wa kibiashara unaandamana na bi Merkel wakati akizuru nchi za Kenya, Nigeria na Angola.
Nchini Kenya Chancela wa Ujerumani ananuia kujadili jinsi ya kuimarisha nishati ya mvuke ambayo inaonekana kupunguza hewa ya Carbon inayolaumiwa kwa ongezeko la viwango vya joto.
katika nchi za Angola na Nigeria Angela Merkel anatarajia kulenga sekta ya nishati hususan mafuta na teknolojia ya mawasiliano.
Aidha mataifa haya yanatarajia kuwasilisha hoja zao hususan uwakilishi wa bara Afrika katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo Ujerumani huwa mwanachama wa kudumu.
Afrika imesisitiza kupewa nafasi ya kudumu hasa kutokana na mchango wake wa karibuni katika jamii ya kimataifa
No comments: