UWANJA WA NDEGE WA SONGWE HUENDA USIKAMILIKE KWA WAKATI
LICHA ya Serikali kuitaka kampuni ya Kundan Singh Construction kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya katika kipindi cha miezi sita ijayo, Uwanja huo hautaweza kukamilika kwa kipindi hicho, Mtandao huu umebaini.
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi kushoto akiwa uwanjani hapo na Afisa wa kampuni ya Kundan Paul Omindo.
Uchunguzi uliofanywa na mtandao huu katika uwanja huo, umebaini kuwa wakati ujenzi huo ukiendelea tayari vifaa na malighafi ya ujenzi wake vinaibwa kwa kasi kubwa ambapo hivi karibuni zimeibiwa pipa kadhaa za lami.
Baadhi ya pipa zenye shehena za lami zilizoibiwa na kukamatwa zimehifadhiwa katika kituo kidogo cha Polisi cha mjini Mbalizi.
Shehena hiyo ya lami ipo katika gari aina ya Land Rover lenye namba za usajili T 780 ALR.
Viongozi wa Kampuni ya Kundan wamethibitisha kuwa shehena hiyo iliibiwa uwanjani hapo hivi karibuni na suala hilo lipo mikononi mwa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya.
Jitihada za kumpata Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi zinaendelea ili kujua hatima ya wahusika.
No comments: