Header Ads

Breaking News
recent

MCHORA KATUNI AVUNJWA MKONO KWA KUMCHORA RAIS

NewsImages/5911250.jpg
Mchora Katuni Ali Farzat



Mchora katuni wa nchini Syria ambaye ni maarufu sana kwa kuchora katuni za kuwakosoa viongozi wa kiarabu, amevunjwa mikono yake baada ya kuchora katuni ya rais wa Syria akiomba akimuomba lifti Gaddafi.
Mchora Katuni Ali Farzat alijipatia umaarufu sana kwa kuchora katuni za kuwakosoa wanasiasa wa nchi za kiarabu.

Kutokana na katuni zake aliwahi kutishiwa kuuliwa na aliyekuwa rais wa Iraq, Saddam Hussein baada ya kuchora katuni za kuuukosoa utawala wake enzi hizo.

Hivi karibuni Farzat mwenye umri wa miaka 60, alichora katuni ambayo ilimuonyesha rais wa Syria, Bashar al-Assad akiomba lifti toka kwa Gaddafi ambaye ameingia mafichoni baada ya serikali yake kuangushwa.

Rais Bashar al-Assad wa Syria huenda naye akaangushwa kama Gaddafi kufuatia mapigano ya kuiangusha serikali yake yanayoendelea nchini humo.

Jioni ya siku ya alhamisi, Farzat alitekwa na watu walioficha sura zao kwa vitambaa na kuingizwa kwenye gari.

Watekaji hao walimwambia Farzat kuwa wataivunja mifupa ya mikono yake ili asiweze tena kuchora katuni.

Waliivunja mifupa ya mikono yake na kisha kumtupa pembeni ya barabara huku wakimwambia kuwa "Hilo ni onyo tu".

Mmoja wa marafiki wa Farzat alisema kuwa ndevu za Farzat nazo zilichomwa moto huku akiambiwa "Tutaona sasa utachora nini, kwanini unajifanya hutii viongozi wako".

Tukio hili limekuja wakati serikali ya Syria ikijaribu kuwatokomeza wasanii na watu wanaoipinga serikali ya rais Assad.

Mwezi uliopita, msanii maarufu aliyetunga wimbo maarufu wa kuipinga serikali alikutwa amefariki kwenye mji wa Hama huku koromeo lake likiwa limenyofolewa.

No comments:

Powered by Blogger.