BASTOLA YA RAGE YAMGHARIMU LAKI
MBUNGE WA TABORA MJINI KWA TIKETI YA CCM ISMAIL ADEN RAGE AMETAKIWA KULIPA SHILINGI LAKI MOJA KAMA FAINI KUTOKANA NA KUPANDA KATIKA JUKWAA LA KAMPENI HUKO IGUNGA MKOANI TABORA AKIWA NA BASTOLA KIUNONI
MBUNGE HUYO AMEPIGWA FAINI HIYO NA KAMATI YA MAADILI YA UCHAGUZI IGUNGA CHINI YA MWENYEKITI WAKE BWANA PROTACE MAGAYANE
MWENYEKITI HUYO PIA AMESEMA KUWA KAMATI YAKE IMETOA KARIPIO KALI LA MAANDISHI DHIDI YA CHADEMA KUHUSU MALALAMIKO KUTOKA KA CCM KUHUSU KUFANYIWA VURUGU NA CHADEMA KATIKA KAMPENI
No comments: