Header Ads

Breaking News
recent

MSHITAKIWA AKOJOA MAHAKAMANI




Kijana mweusi mwenye umri wa miaka 17 wa nchini Marekani alimuudhi hakimu pale alipoamua kusaula nguo zake na kukojoa mahakamani mbele ya umati wa watu waliokuwepo mahakamani kusikiliza kesi hiyo.

Kijana huyo aliyetajwa kwa jina la Corey Webb alifikishwa mahakamani kwa kumpiga risasi afisa wa polisi wakati alipokuwa akiwazuia kutoroka toka kwenye jela ya watoto.

Webb kabla ya kuamua kukojoa mahakamani alikuwa akifanya vituko mbali mbali kama vile kupiga kelele wakati akisomewa mashtaka yake. Aliwashangaza watu alipomtaka hakimu amfukuze wakili aliyekuwa akimtetea.

"Sijui umelelewaje lakini kukojoa kwenye pipa la taka ndani ya mahakama ni tabia mbaya", alisema jaji baada ya Webb kuteremsha nguo zake na kukojoa ndani ya mahakama.

Kesi iliahirishwa hadi siku nyingine.

No comments:

Powered by Blogger.