AMA KWELI DIMBA HIZI ZA QATAR WORLD CUP 2022 ZINATISHA.
Uwanja wa Ahmed bin Ali, maarufu kama Al-Rayyan Stadium - ni uwanja unaotumika katika mambo mengii.
Lakini uwanja huu utatfanyiwa marekebisho upya kwa ajili ya World Cup 2022, na kuweza kuchukua watazamaji wakiwa wamekaa kwenye viti 44,740.
Uwanja wa AL-Wakrah ni uwanja unaotumika kwa michezo mingi katika mji wa Al Wakrah, Qatar. Kwa sasa unatumika zaidi kwa ajili ya kuchezea soka. Uwanja huu unachukua watazamaji 20,000 lakini utatengenzwa na kuweza kuchukua watazamaji 43,500.
Uwanja huu unaitwa AL-Khor utakuwa unaingiza watu wapatao 45,000, pamoja na siti nyingine za ziada 1000 kwa ajili ya waandishi wa habari.
Pia dimba hili litakuwa na parking ya kuhimili magari 6,000, mabasi 350, pia sehemu ya kuingia na kutoka ya mabasi ya abiria yapatayo 150 kwa wakati mmoja.
Education City Stadium, ni uwanja ambao utajengwa mjini Doha -Qatar, kwa ajili ya World Cup 2022.
Lusail Iconic Stadium, ni uwanja ambao utajengwa hapo baadae katika mji wa Lusail. Huu ndio uwanja utakaotumika kwa ajili ya mechi za ufunguzi na fainali za World Cup 2002.
Uwanja huo utajengwa kwenye maji na utakuwa umeunganishwa na madaraja 6 ambayo yatakuwa yakielekea uwanjani. Umebuniwa na Waingereza wajiitao Foster + Partners.
Sports City Stadium ni uwanja ambao nao utajengwa maalum kwa kombe la dunia in 2022. Utakuwa mjini Doha Qatar. Utakuwa na uwezo wa kuingiza watu wasiopungua 42,000. Uwanja huu utakuwa na teknolojia ya hali juu ya kupambana na hali ya joto kubwa liliopo katika nchi hiyo.
Umm Salal Stadium utakuwa ni uwanja wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 45,120. Uwanja huu umebuniwa katika mila ya ngome za kiarabu. Baada ya World Cup 2022, uwanja huu utatumika na klabu ya Umm Salal FC kama uwanja wao wa nyumbani.
No comments: