DAWA YA MAMBA WALA WATU YAPATIKANA SASA KUJENGWA UKINGO KANDOKANDO MWA ZIWA VICTORIA.
HATIMAYE HALIMASHAURI YA JIJI LA MWANZA IMESIKIA KILIO CHA WAKAZI WA MAENEO YA KANDOKANDO YA ZIWA KWA KUIDHINISHA UJENZI WA UZIO MAALUMU KUZUNGUKA VITUO MBALIMBALI VYA KUVULIA SAMAKI ILI KUDHIBITI ONGEZEKO LA MATUKIO YA MAMBA KUWALA WATU KATIKA MAENEO HAYO.
HAYO YAMEJIRI KATIKA MKUTANO ULIOFANYIKA MAPEMA LEO, KATI YA MKURUGENZI WA JIJI LA MWANZA, BWANA WILSON KABWE, NA WAANDISHI KUTOKA VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI JIJINI HUMO.
BWANA KABWE AMEELEZA KUWA HALMASHAURI YAKE IMELENGA KUJENGA JUMLA YA VITUO KUMI NA VITANO KATIKA ENEO LOTE LA KANDA YA ZIWA, AMBAPO PAMOJA NA MAMBO MENGINE, WAMEANZA NA KITUO CHA BWIRU.
AMEENDELEA KUDOKEZA KUWA UJENZI HUO UNATEKELEZWA KUFUATIA WITO ULIOTOLEWA NA CHAMA CHA WAVUVI CHA KANDA YA ZIWA KILICHOIOMBA HALIMASHAURI HIYO KUINGILIA KATI NA KUYANUSURU MAISHA YAO KWA KUIDHINISHA UJENZI WA UZIO KATIKA MAENEO TAJWA.
AMEFAFANUA KUWA HALIMASHAURI YAKE ITASHIRIKIANA NA WAJASIRI AMALI HAO KATIKA KUHAKIKISHA KUWA WANAFANYA SHUGHULI ZAO KWA USALAMA HUKU WAKIWADHIBITI MAMBA HAO HATA WASIWEZE KUTOKA NCHI KAVU.
SAKATA LA MAMBA KUWALA WATU KATIKA MAENEO YANAYOZUNGUKA ZIWA VICTORIA, LIMEKUWA LA MUDA MREFU AMBAPO MWISHONI MWA MWAKA JANA ZAIDI YA WAVUVI WATANO WALIRIPOTIWA KULIWA NA MAMBA HUKU WENGINE KUMI NA WATANO WAKIARIFIWA KUJERUHIWA VIBAYA.
MAMBA HAO WAMERIPOTIWA KUTOKA NCHI KAVU NYAKATI ZA USIKU, MUDA UNAOTUMIWA NA WAVUVI KATIKA UVUVI, ILI KUKUSANYIKA KABLA YA KUHITIMISHA SHUGHULI ZAO NA KUREJEA MAJUMBANI MWAO.
LICHA YA UVUVI KUTAJWA KAMA MHIMILI WA UCHUMI KWA WAKAZI WENGI WA KANDA YA ZIWA, BADO SAMAKI WAMETUMIKA KAMA VITOWEO, AMBAPO PAMOJA NA MAMBO MENGINE, HUPUNGUZA MAKALI YA MAISHA KATIKA ENEO HILO.
No comments: