MTOTO WA GADDAFI-SAAD GADDAFI AKIWA UHAMISHONI NCHINI NIGER ATABIRI KUZUKA MAPIGANO MAPYA LIBYA
MAMLAKA MPYA YA MPITO YA LIBYA IMEITAKA SERIKALI YA NIGER KUINGILIA KATI NA KUMDHIBITI MWANA WA KIUME WA ALIYEKUWA MUAMMAR ABUU MINYAR AL - GADDAFI KUHUSU KAULI TATANISHI ANAZOZITOA DHIDI YA USALAMA WA LIBYA.
HAYO YAMEJIRI KUFUATIA MAHOJIANO YALIYOFANYIKA KATI YA BWANA, SAADI GADDAFI NA TELEVISHENI MOJA YA KIARABU, AMBAPO MAJERUHI HUYO WA SIASA ZA UPINZANI AMETISHIA KUONGOZA VITA DHIDI YA SERIKALI YA BENGAZI.
BWANA SAADI AMETABIRI KUZUKA KWA MAPIGANO KADHAA KATIKA MAENEO MBALIMBALI YA NCHI HIYO KUFUATIA MAWASILIANO YA KARIBU KATI YAKE MAKUNDI KADHAA NDANI YA LIBYA.
BWANA SAADI, ALIYEKIMBILIA NCHINI NIGER MUDA MFUPI BAADA YA ILIYOKUWA SERIKALI YA BABA KUPINDULIWA MAPEMA AGOSTI MWAKA JANA, AMENUKURIWA AKIELEZEA TARAJA YAKE YA KUREJEA NCHINI HUMO MUDA MFUPI UJAO.
No comments: