Header Ads

Breaking News
recent

KASEJA:KESHO MASHABIKI WETU TUTAWAFUTA MACHOZI KWA AZAM


                                juma .k.juma

NAHODHA wa Simba, Juma Kaseja, amesema wachezaji watawafuta machozi washabiki kwenye mechi dhidi ya Azam Jumapili ijayo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kaseja alisema wachezaji wa Simba wanajua maumivu waliyonayo washabiki mara baada ya kupoteza mechi dhidi ya Villa Squad na ndiyo maana wanataka kurekebisha mambo.
Katika mchezo wao jumamosi iliyopita, Simba   ilifungwa na Villa bao 1-0 katika pambano lililofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini, matokeo ambayo yaliwauma washabiki wengi ikizingatiwa kuwa timu hiyo ndiyo inayoshika mkia kwenye ligi.

“Soka ni mchezo wa ajabu sana kuna wakati kunakuwa na matokeo ambayo hakuna anayeyategemea,ila mimi namwamini MUNGU kuwa kuna wakati  naye anakuwa na mipango yake,Alipangalo Mungu haliepukiki,” alisema.
Hata hivyo, Kaseja alisema ana imani Mashabiki watasahau kuhusu mchezo wa Villa iwapo Simba itaibuka mshindi katika pambano gumu dhidi ya Azam Jumapili ijayo.
Alisema ndiyo maana sasa wachezaji wote wa Simba wameleekeza nguvu zao zote katika pambano hilo wakifahamu fika kuwa matokeo ya mchezo huo yakiwa mazuri, Simba itatulia.

No comments:

Powered by Blogger.