Header Ads

Breaking News
recent

KIONGOZI NA MSHINDI WA TUZO YA DHAHABU YA LONDON 2012 LORD SEBASTIAN CEO AIZULU TANZANIA.


Kiongozi wa Olimpiki London 2012 Bw. Lord Sebastian Ceo akiwa katika picha ya pamoja na watoto baada ya kuwakabidhi vyeti katika ziara maalum aliyoifanya nchini Tanzania na kutembelea shule ya Sekondari ya Kibasila, ambako kuliandaliwa kliniki ya watoto kwa kuvumbua vipaji na kuwaandaa kwa ajili ya michezo ya Olimpiki katika siku za usoni, iliyojulikana kama Interanational Inspiration Tanzania na kushirikisha watoto kutoka shule mbalimbali jijini Dar es salaam, hapa wakionyesha vyeti vyao mara baada ya kukabidhiwa vyeti vyao na kiongozi huyo.
Kiongozi wa Olimpiki London 2012 Bw. Lord Sebastian Ceo akiruka viunzi pamoja na mtoto Aica Nicolaus wakati wa kiliniki hiyo kwenye viwanja vya shule ya Sekondari ya Kibasila.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kibasila wakicheza ngoma kumkaribisha kiongozi wa Olimpiki London 2012 Bw. Lord Sebastian Ceo.
Mmoja wa watoto akirusha Tufe mbele ya Kiongozi wa Olimpiki London 2012 Bw. Lord Sebastian Ceo wa tano kutoka kulia, hyuku viongozi wengine kutoka kamati ya Olimpiki nchini na Baraza la Michezo na ubalozi wa Uingereza nchini wakishuhudia tukio hilo.
Kiongozi wa Olimpiki London 2012 Bw. Lord Sebastian Ceo kulia akiangalia watoto wakati walipokuwa wakifanya mazoezi ya kuruka viunzi anayefuata katika picha ni Dk. Ndee na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki Tanzania TOC, Filbert Bay.

Watoto wakifanya mazoezi
Kutoka kulia ni Julie, Nelly Musembi na Vickie Maundu nao walihudhurika katika kiliniki hiyo ya International Inspiration Tanzania
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kibasila Mrs Aikande Urasa akimuongoza mgeni ambaye ni Kiongozi wa Olimpiki London 2012 Bw. Lord Sebastian Ceo kulia alipowasili katika shule hiyo katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya Olimpiki Tanzania TOC, Filbert Bay

No comments:

Powered by Blogger.