SAKATA LA MGAO WA UMEME SASA LIMEKWISHA.
WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja, amesema kwa sasa tatizo la mgawo wa umeme
limekwisha kwa kuwa mitambo yote ya Serikali na binafsi inazalisha megawati nyingi kuliko mahitaji.
Akizungumza na mwandishi wa safu hii ya msasa wa wiki ofisini kwake mjini Dodoma juzi, alisema kwa sasa mitambo hiyo inazalisha megawati za umeme 1,028.70 wakati mahitaji ya juu kwa wastani wa mwezi ni megawati 821.
Ngeleja alisema si kweli kwamba Serikali imeshindwa kudhibiti tatizo la mgawo kwani ulishadhibitiwa tangu Oktoba mwaka jana na sasa kinachoendelea ni kuhakikisha haurejei tena nchini.
“Uwezo wa kuzalisha umeme kwa sasa umezidi kuliko mahitaji, kwa mwezi mzima uliopita mahitaji yalikuwa yanacheza kwenye megawati 821 wakati mahitaji ya juu kwa jana pekee (juzi) yalikuwa megawati 717.60.
Aliwataka wananchi kutambua kuwa umeme unapokatika katika maeneo yao haimaanishi kuwa ni mgawo, bali wakati mwingine hutokana na hitilafu za kawaida za kiufundi.
“Kwa sasa kama Serikali tumejidhatiti kuhakikisha kuwa mgawo haurejei tena nchini, kwani pamoja na kuzalisha sasa nyongeza ya megawati 321.10 kuliko mahitaji kuna miradi mingine iko mbioni kukamilika,” alisema.
Alisema moja ya miradi hiyo ni pamoja na bomba la gesi linalotarajiwa kufungwa kutoka Mnazi Bay mkoani Mtwara hadi Dar es Salaam ambalo likikamilika mwakani kama inavyotarajiwa, litazalisha megawati za umeme 3,000.
Ngeleja alisema hayo kutokana na taarifa zilizozagaa kuwa Serikali imeshindwa kudhibiti mgawo wa umeme na kwamba bado kuna baadhi ya maeneo unaendelea chinichini hususani katika mkoa wa mwanza.

No comments: