MAMAA KIZAAZAA HICHOOOOO ,KIJANA AIBA SIMU SASA INALIA TUMBONI MWAKE-MBALIZI[MBEYA].
KATIKATI NI MWENYEKITI WA KIJIJI CHA MBALIZI ELIA MKONO AKIWA ANAFAFANUA JAMBO KWA MKUU WA WILAYA HIYO EVANCE BALAMA.
KIJANA mmoja mkazi wa mji mdogo wa Mbalizmkoani mbeya anateseka kwa kusikika kwa mlio wa simu unaotoka tumboni mwake.
Kijana huyo ambaye ni mbeba mizigo katika stendi ya Mbalizi anayejulikana kwa jina la Subi Andendekisye Mwaipopo amekumbwa na mkasa huo leo ambapo mlio huo wa simu unasikika ukisema kuwa rudisha simu yetu na wakubwa zako waeleze haraka.
Akizungumza na chombo kimoja cha habari kwa njia ya simu SUBI amekiri kuwa na tatizo hilo lakini amekana kuhusika na wizi wa simu hiyo.
Amesema kuwa tatizo hilo halijaanza leo bali ni la muda mrefu ambapo amekuwa akisikia sauti kutoka tumboni mwake mtu akisema kuwa arejeshe simu na fedha jambo ambalo amedai kuwa linampa shida sana.
Alipohojiwa kuwa atawezaje kujinasua katika dhoruba hiyo kali amesema hana namna ya kufanya kwa sababu anaamini kuwa hata akienda hospitalini hawezi kupata tiba na kwamba kila sauti hiyo inapoanza kusikika hujihisi kuwa amepatwa na malaria.
No comments: