Header Ads

Breaking News
recent

MAMLAKA YA HALI YA HEWA YA FUNGUA RASMI MAFUNZO KWA WADAU WAKE MKOANI MWANZA


 Mamlaka ya hali ya hewa nchini imefungua rasimi mafunzo  yaliyoanza jana kwa wadau wa huduma ya hali ya hewa katika maeneo  ya ziwa victoria ,Huku ikishirikisha wakulima,wafugaji,wavuvi ,wasafirishaji na wanahabari nchini.

 
Mkuremkurugenzi wa mamlaka ya hali ya hewa nchini tanzania Dr,Agnes Kijazi,akifungua Mafunzo ya wadau wa mamlaka hayo (Hawako pichani)Mkoani Mwanza

Kaimu katibu tawala Mkoani Mwanza mhandisi warioba sanya akisoma taalifa ya Mamlaka ya hali ya hewa kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza

Wadau katika picha ya pamoja Baada ya Ufunguzi wa mamlaka hiyo



Na  Mwandishi wetu,MWANZA

Mamlaka ya hali ya hewa nchini imefungua rasimi mafunzo  yaliyo anza jana kwa wadau wa huduma ya hali ya hewa katika maeneo  ya ziwa victoria ,Huku ikishirikisha wakulima,wafugaji,wavuvi ,wasafirishaji na wanahabari nchini.

akisoma taarifa ya  mgeni rasimi  mkuu wa mkoa ,kaimu katibu tawala  mhandisi warioba sanya,katika ufunguzi wa  warsha,amewaagiza wajumbe wa warsha hiyo kutumia mradi huo kuhakikisha wanapanua wigo wa usambazaji wa taarifa za hali ya hewa katika ukanda wa ziwa viktoria na maeneo jirani ya eneo hilo.


Hata hivyo,mhandisi  Sanya amewataka watendaji wa malaka ya hali ya hewa nchini kuendelea kutoa huduma za hali ya hewa kwa ufanisi mkubwa na kuendelea kuboresha kwa kina taarifa hizi  kwa lengo la kuwasaidia wananchi na kuwapatia elimu ya kutosha juu ya mamlaka ya hali ya hewa nchini.


kwa upande wake mkurugenzi wa mamlaka ya hali ya hewa nchini tanzania dkt,agnes kijazi,amesema kuwa kupitia mradi huo wa kutoa taarifa kwa njia ya simu za mkononi wamefanikisha kupata jumla ya namba za simu ya mkononi kwa wakazi  350 wa wilaya ya sengerema ambao watasaidia kutumiwa ujumbe wa kupewa tarifa na kisha kufikisha kwa wananchi ambao watakuwa bado hawajapatiwa taarifa za utabili.


Nao  wadau walio shiriki semina hiyo wameipongeza mamlaka ya hali ya hewa kwa kuanzisha huduma hiyo kwani kwa sasa itakuwa ni raisi kwa wao kufikiwa na taarifa juu ya mabadiriko ya hali ya nchi na mamlaka ya hali ya hewa kwa ujumla.







No comments:

Powered by Blogger.