MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA UONGOZI WA NEC-JAPAN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mheshimiwa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal leo amekutana
na Uongozi wa Kampuni ya NEC yenye makao yake makuu jijini Tokyo nchini
Japan. Ujumbe wa NEC-Japan umeongozwa na Rais wa Kampuni hiyo
inayojishughulisha na masuala ya Mawasiliano na Teknolojia, Dkt.
Nobuhiro Endo.
Ujio wa Kampuni hii nchini
Tanzania unatokana na mwaliko wa Tanzania kwa makampuni ya Japan
kufuatia ziara ya kikazi aliyoifanya Mheshimiwa Makamu wa Rais nchini
Japan, mwezi wa Mei mwaka huu. Mheshimiwa Makamu wa Rais alitembelea
Makao Makuu ya Kampuni hiyo wakati za ziara hiyo.
Katika mazungumzo na uongozi wa
NEC Mheshimiwa Makamu wa Rais aliwaeleza wageni wake nia ya Tanzania
kuona inatanua mawasiliano na teknolojia nchini ili kuinua uchumi na
akafafanua kuwa teknolojia yoyote kutoka NEC inakaribishwa hapa nchini
ili kusaidia Tanzania kupiga hatua.
Uongozi wa NEC nao ulimueleza
Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa, NEC inaushirikiano wa karibu na Shirika
la Simu Tanzania (TTCL) na kwamba wanatarajia kukutana na uongozi wa
wizara ya Mambo ya Ndani kwa lengo la kutazama fursa za kusaidia
teknolojia katika ulinzi.
Imetolewa na:
Ofisi ya Makamu wa Rais
Ikulu Dar es Salaam Septemba 12, 2014
No comments: