DOVUTWA NAYE AWASHANGAA UKAWA
Dodoma
Mwenyekiti
wa Chama cha UPDP Taifa , na Mjumbe wa Bunge Maalum la
Katiba, Fahmi Dovuta amesema anawashangaa viongozi wanaojiita UKAWA
kwa kumwita msaliti, huku akihoji kwamba anawezaje kukihujumu chama chake na
vinginneyo.
Kauli
hiyo ilitolewa leo na Mwenyekiti huyo mjini Dodoma wakati kikao cha
Thelasini na Tisa cha Bunge hilo, linaloendelea mjini huo kujadili sura za
Rasimu Mpya ya Katiba zilizobakia na sura mpya.
“
Nimepokea simu mara tatu za vitisho, kwamba watanifanyizia.
“ Wenzetu
hawa kama walikuwa hawakubaliani , walikuwa na nafasi
ya kuomba mashauriano halafu wakesema hayo wanayoyasema,” .alisema
Dovutwa.
Aliongeza
kuwa katika kikao cha Viongozi Wakuu wa Vyama vya Siasa
vyenye wabunge vinavyounda Kituo cha Demokrasia
nchini(TCD) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. Jakaya Kikwete .
Dovutwa
ambaye ni mwakilishi wa vyama vya siasa visivyokuwa na wabunge Bungeni,
alifafanua kwamba katika kikao hicho, cha Septemba 8, mwaka 2014
mambo waliyokubaliana ni kwanza kufanya marekebisho kuhusu Uchaguzi Mkuu
wa mwaka 2015 na kuhusu usitishwaji wa Bunge hilo, hakuna mwenye mamlaka
kisheria.
Aliendelea
kuelezea kuwa katika kikao cha Agosti 31, mwaka 2014 Tundu Lissu alimtaka
Rais Kikwete kusitisha Bunge hilo, lakini Rais Kikwete akamjibu yeye
ndiye aliyetaka (Rais) asiwepo katika Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba, huku akimhoji kuwa amwonyeshe sheria
atakayoitumia.Aliongeza kwamba Lissu hakuwa na la kusema.
Dovutwa
alisema walikubaliana kwamba waje katika Bunge hilo, lakini wanaona
kuganyaga mlango wa wa Bunge hilo ni ugumu kama kurudia
‘kunyonya, kama hawataki kuzungumza mbele ya wenzetu… nani wa kulaumiwa,’
alisisitiza.
Aidha
Dovutwa alisema katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika hivi
karibuni, ilikuwa viongozi hao na waje kwa ajili ya kutoa tamko la
kuhusu makubaliano ya kikao hicho, lakini hawakutokea.
“Hili ni
jambo baya linaleta chuku na uchonganishi wa halai ya juu,” alisema Dovutwa.
Akizungumzia
kuhusu suala la kukataa kusaini , alisema walijua ilikuwa ni mtego kwa
vile walipewa maelezon wasaini dakika chache kabla ya kuingia katika kikao
hicho, hivyo hawakuwa na muda wa kusoma.
Alisema
pia walibaini kuna kipengele cha hatari cha kutaka Bunge lisitishwe.
chanzo:fullshangwe
No comments: