STARKEY HEARING FOUNDATION KUTOKA MAREKANI KUENDESHA KLINIKI MAALUMU KWA WATU WENYE USIKIVU HAFIFU
Shirika lisilo la kiserikali la starkey hearing foundation kutoka marekani
linatarajia kuendesha kliniki maalumu kwa watu wenye usikivu hafifu jijini Mwanza
kuanzia tarehe 19 septemba hadi septemba
21 mwaka huu mkoani Mwanza.
akizungumza na kwaneema fm radio
mkurugenzi wa shirika hilo Bwana Yohana Lubango ambaye ni mwalimu wa elimu
maalumu,amesema kuwa lengo la shirika hilo ni kuwasaidia watu wasio sikia na
wale wenye matatizo ya masikio hususani watoto ambao wameathiriwa na mionzi ya
simu.
Kwa upande wake Bwana William Charles amesema kuwa uchunguzi huo utatolewa kwa muda
wa siku tatu katika shule ya msingi nyanza na itatolewa bure kwa watu wote.
shirika la starkey hearing
foundation limekuwa likitoa huduma ya kupima masikio katika bara la afrika na
kutoa matibabu ya awali kwa watu wanao onekana kuwa na tatizo hilo.
CHANZO: Mahojiano na joel Maduka
No comments: