KWA NEEMA FM RADIO YAPATA MKURUGENZI MPYA
Bwn: PETER OMARY ambaye ni mkurugenzi mpya wa kwa neema fm akiwa katika pozi.
NA: Mv. Jacktan
Uongozi wa
kituo cha redio kwaneema fm cha jijini mwanza umemtangaza bwn:Peter Omary kuwa mkurugenzi mtendaji wa
kituo hicho ambaye atakuwa mtendaji mkuu katika uendeshaji wa redio hiyo.
Bwn: Peter
Omary anachukua nafasi hiyo ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Askofu mkuu wa
kanisa la TFE kwaneema bishop Augastine Mpemba ambaye yuko nje ya nchi kimasomo kwa muda mrefu sasa.
Akizungumza
muda mfupi baada ya kutangazwa rasmi mbele ya wafanyakazi wa kituo hicho Bwn:
Omary amesema atahakikisha kituo hicho kinawanufaisha watanzania walio wengi
kutokana na mikakati mipya mbalimbali ilofikiwa ikiwa ni pamoja na kupitia upya
vipindi vya redio kwa lengo la kuviboresha zaidi.
Aidha Bwn:
Omary amewataka wasikilizaji wa 98.2 kwaneema fm radio kuendelea kukiunga mkono
kituo hicho likiwemo tamasha la miaka 5 tangu kuanzishwa kwake litakalofanyika
JB Belmont hotel 6/4/2015 kwa kuendelea kununua tiketi kwa wingi, ambapo pia amesema
hakuna kitakachobadilika bali ubora wa kituo kuongezeka kwa kasi siku hadi
siku.
wafanyakazi wa kwaneema fm radio wakiwa kwenye picha ya pamoja na mkurugenzi mpya.
Marium Juma Mtaalamu wa masoko akiwa na mkurugenzi
Program menegerJackline Raphael akiwa na mkurugenzi
Mtaalamu wa kipindi cha full shangwe extra Joshua Dede akiwa na mkurugenzi
Chief Editor Jeston Kihwelo akiwa na mkurugenzi
Mwanahabari Dominic Felician akiwa na mkurugenzi
Mtaalamu wa blog na mitandao Mv.jacktan akiwa na mkurugenzi
Meneja wa redio Evelyne Endrew akiwa na mkurugenzi
Mtaalamu wa kipindi cha yaliyosheheni Specyoza Haule akiwa na mkurugenzi
Mtaalamu mwingine wa kipindi cha full shangwe extra Fabian Fanuel akiwa na mkurugenzi
No comments: