WAZUNGU wawili wenye asili ya uingereza walikamatwa na nyara za serikali.
Tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 30 june mwaka huu wakati askari wa idara ya uhamiaji wilayani humo wakiwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Walifanikiwa kuwakamata NICHOLAUS VIDMR. Na HOUS CHABERS,Wakiwa na nyara za serikali pembe nne za tembo,
Waingereza hao walifikishwa mahakamani jana tarehe 8 Julai mwaka huu katika mahakama ya hakimu mfawidhi Mkoa wa Mbeya.
Mwendesha mashitaka wa polisi GRIFFIN MWAKAPEJE. Aliwasomea shitaka hilo mbele ya hakimu mfawidhi wa mkoa wa Mbeya ZABIBU MPANGULE.
Washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kutokana na kosa hilo ambalo ni uhujumu uchumi, washitakiwa wote walipelekwa rumande hadi tarehe 21 julai mwaka huu itakapotajwa tena.
Wakati huo huo Jeshi la Polisi Mkoani Imeanzisha msako kwa watu waliohusika kumuua Mwalimu JUMA said.
Akizungumza Waandishi wa Habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi alisema JUMA SAID (56) aliyekuwa mwalimu wa shule ya msingi Utengule aliuwa na watu awasiojulikana Julai 7 saa 2.33 usiku akiwa nyumbani kwake utengule Mbalali Kamanda Nyombi alisema marehemu ambayepia alikuwa mfanyabiashara.
''Baada ya kuvamiwa na majambazi alapigwa risasi mbili kwenye paja kabla ya kuporwa pesa ambazo hazikujulikana thamani yake, Msako mkali na tunaomba ushirikiano kutoka kwa wananchi,alisema Kamanda Nyombi.
No comments: