Header Ads

Breaking News
recent

VIWEMBE VYA TUMIKA KUONGEZA HAJAKUBWA BAADA YA MTOTO KUZALIWA AKIWA HANA SEHEMU HIYO MKOANI MWANZA

BI: ANASTAZIA NGILITU AKIWA NA MWANAYE AMBAYE ALIMCHANA KWA VIWEMBE KUPATA SEHEMU YA HAJA KUBWA.



MWANZA,na Stela B




Vitendo vya baadhi ya wananchi kujitibu pasipo kufuata maagizo na njia za kitaalamu vimeendelea kukithiri nchini ambapo hapa jijini Mwanza mama mmoja ameamua kumchanja kwa viwembe mwanae mwenye umri wa wiki mbili baada ya  mtoto huyo kuzaliwa akiwa hana sehemu ya Haja kubwa.

Tukio hilo limetokea hivi karibuni baada ya mama huyo aliyefahamika kwa jina la Anastazia Ngilitu kumchana kwa wembe zaidi ya mara tatu ili kumsaidia mwanae kupata haja kubwa kwa kile kilichodaiwa mtoto huyo kuzaliwa akiwa hana sehemu  ya haja kubwa.

Katika mahojiano maalumu namama huyo mkazi wa Tabora aishie jiini mwanza kwa sasa amesema kuwa alijifungua watoto mapacha watatu ndani ya Mtaro kisha wawili kufariki alipofikswa Hospitali na kusalia mtoto mmoja aliyekutwa na tatizo la kutokua na sehemu ya haja kubwa.

Sambamba na hayo mama huyo amesema kuwa sababu za kumchana na wembe mwanawe ni baada ya kumuona mtoto wake anashindwa kupata haja kubwa hali 
inayopelekea tumbo kujaa na kulia.

Ameongeza kuwa wakati wa kujifungua mtoto huyo walimfanyia upasuaji katika hospitali ya Bugando ila hali ya kuziba ilijirudia tena na kuamua kumchana kwa 
kutoakana na kutokuwa na uwezo wa kulipia gharama za upasuaji hospitali.

Katika hatua nyingine Mama huyo amesema kuwa kwa sasa hali yake ya Maisha siyo nzuri kwani watoto wake wanaishi kwa kunywa maji na kwamba hapo awali alikuwa anafanya kazi ya kufua nguo kwenye nyumba za watu ila kwa sasa hawezi kutokana na kuwa na motto mdogo.

Sambamba na hayo mama huyu anasema kuwa licha ya kuolewa na wanaume watatu kwa wakati tofauti na kila mmoja kumnyanyasa kwa kumpiga na mwingine kumdhurumu pesa zaidi amesikitishwa na kitendo cha Mume wake wa sasa hivi kumtaka kufanya mapenzi ikiwa tumbo la uzazi halijakaza hali anayotaja kumsababishia maumivu makali na kutokwa na damu nyingi baada ya mumewe kumpiga.

Kitendo cha mama huyu kumchana mtoto wake kwa wembe kinatokana na hofu ya kwenda hospitali kwani anasema hana uwezo wa pesa kwani kwa sasa yeye mwenyewe anasumbuliwa na uvimbe katika titi lake la kushoto na alipoenda Hospitali ya SEKOTURE aliambiwa gharama za upasuaji ni shilingi elfu 30 nakwamba alipokosa alirudi nyumbani na kuendelea kujitibu kwa dawa za kienyeji.

Kwa upande wao baadhi ya  majirani ambao wamekuwa wakimpa msaada mama huyu mara kwa mara,Wamesema mama huyo ana maisha magumu kwani mume wake humpiga na kumfukuza mara kwa mara hali inayomfanya aishi kwa kuomba omba na wakati mwingine kulala na watoto wake 
bila kula.

Taarifa za awali zinaonyesha kuwa mama huyu aliolewa na mume wa kwanza mkazi wa eneo la maji moto mkoani Mara na waliachana baada ya kupigwa na kuchomwa kisu tumboni ikiwa ni pamoja na kupigiliwa msumali wa nchi sita katikati ya mkono  wake wa kushoto ikiwa ni sambamba na kumvuta hereni akimwambia kuwa ni dalili za kuwa malaya hali iliyomsababibishia masikio yake kuvimba.

Mume wa pili aliyemuoa mama huyo inaelezwa kuwa yeye alimdhurumu kiwanja walichouza milioni moja na laki saba kilichokuwa eneo la makaburi Bwiru kisha 
kuzichukua na kuaga kwenda kuzifanyia biashara.

Kuhusu ndugu Bi Anastazia amesema kuwa wazazi wake wote wamefariki na kwamba aliyebaki ni bibi yake ambaye naye anamtaja kuwa ni mchawi kwani wakati alipoenda Tabora,bibi yake alimwambia ampe mkono wa mtoto ili usiku wa manane  amuamshe kwa kumpiga nao kichwani ili aende kazini.

Anastazia anasema kuwa kutokana na matatizo hayo aliwahi kushauriwa kumtupa mtoto huyo eneo la vichakani soko la sabasaba,ushauri aliopewa na rafiki yake mkazi wa Ilemela aliyemtaja kwa jina moja la Amina ambaye alimwambie mtoto wako hatapona,Jambo ambalo yeye alikataa na kusema kuwa anaogopa mkono wa Sheria.

Aidha,Tatizo linalomsumbua mama huyo kwa sasa ni chakula na matibabu kwa mwanaye na yeye mwenyewe anayesumbuliwa na uvimbe katika titi lake la kushoto


No comments:

Powered by Blogger.