Header Ads

Breaking News
recent

YALIYOJILI WIKI JANA MBEYA DODOMA NA ZANZIBAR



TUANZIE MKOANI MBEYA

MAMA MMOJA AMEDAI KUPIGWA NA MUUGUZI WAKATI AKIJIFUNGUA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA META YA JIJINI MBEYA NA MWANAE MCHANGA KUTUPWA KIFUANI MWAKE JAMBO AMBALO LIMEMUATHIRI MTOTO HUYO.

MKUU WA MKOA WA MBEYA BW: AMOS MAKALLA AMEFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA WAZAZI META YA JIJINI MBEYA NA KUSHUHUDIA MSONGAMANO MKUBWA WA AKINA MAMA WAJAWAZITO HOSPITALINI HAPO.



KUFUATIA MADAI HAYO, MKUU WA MKOA WA MBEYA AMOS MAKALLA AMELAZIMIKA KUPITIA NYARAKA ZA MAMA HUYO ILI KUMTAMBUA MUUGUZI ALIYEMFANYIA UKATIRI HUO NA KUMBAINI BI: BEATRICE SANGA ALIYEFANYA UNYAMA HUO.
 
 AIDHA DR: MAKALA AMETOA AGIZO KWA MKURUGENZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI, DR: GOODLOVE MBWANJI KUFANYA UCHUNGUZI NA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA MUUGUZI HUYO NDANI YA SIKU SABA.


MKURUGENZI WA HOSPITALI HIYO, DK. GOODLOVE MBWAJI AMESEMA KUWA KATIKA MAZINGIRA HAYO HAWEZI KUJITETEA NA BADALA YAKE ATAZINGATIA MAELEKEZO AMBAYO AMEPEWA NA MKUU WA MKOA.
NA SASA TUELEKEE KULE DODOMA

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DR: ALI MOHAMED SHEIN AMEAPISHWA KUWA MJUMBE WA BARAZA LA MAWAZIRI ILI AWEZE KUSHIRIKI NA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE NDANI YA BARAZA HILO.



RAIS SHEIN AMEAPISHWA NA JAJI MKUU WA TANZANIA JAJI MOHAMED CHANDE OTHMAN KATIKA IKULU NDOGO YA CHAMWINO MKOANI DODOMA.
 
 TUKIO HILO LIMESHUHUDIWA NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR: JOHN POMBE MAGUFULI.
  
VIONGOZI WENGINE WALIOSHUHUDIA TUKIO HILO NI MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BI: SAMIA SULUHU HASSAN, WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA NA KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI JOHN KIJAZI.

PIA KINGINE KULE DODOMA NI KWAMBA

SERIKALI ITAAJIRI WATUMISHI WA KADA MBALIMBALI ELFU 71 NA 496 KWA MWAKA WA FEDHA 2016/2017.



TAARIFA HIYO IMETOLEWA NA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS, UTUMISHI NA UTAWALA BORA BI: ANGELA KAIRUKI, WAKATI AKIJIBU SWALI LA NYONGEZA LA MBUNGE WA MBULU MJINI BW: ZACHARIA ISSAAY.



MBUNGE HUYO ALIHOJI KUWA NAFASI ZA WATENDAJI WA VIJIJI NA KATA ZIMEKUWA WAZI NI KWANINI SERIKALI ISIONE UMUHIMU WA KUTOA NAFASI KWA VIJANA WALIOMALIZA VYUO KUANZA KUJITOLEA KATIKA KIPINDI CHA MPITO ILI BAADAE WAINGIE KWENYE MFUMO WA AJIRA.
 
KAIRUKI AMESEMA PAMOJA NA UFINYU WA BAJETI, SERIKALI KATIKA MWAKA UJAO WA FEDHA UNAOANZA JULAI, MWAKA HUU, ITAAJIRI WATUMISHI WA KADA MBALIMBALI, WAKIWAMO WATENDAJI WA VIJIJI NA KATA AMBAPO AJIRA ZAO ZITAANZA KUTOLEWA MWEZI HUU.
 
AMESEMA MAOMBI YA NAFASI ZA AJIRA SERIKALINI HUFANYIKA KWA UWAZI KUPITIA BAJETI YA SERIKALI AMBAYO HUIDHINISHWA NA BUNGE.
 
AIDHA,BI: KAIRUKI AMESEMA TANZANIA NI MOJA YA NCHI ZA AFRIKA AMBAZO HULIPA KIMA CHA CHINI CHA MSHAHARA SAWA NA ASILIMIA 80 YA KIWANGO CHA GHARAMA ZA MAISHA.

KUTOKA DODOMA BUNGENI

WABUNGE WANAWAKE WA UPINZANI WAMETOKA WOTE NJE YA BUNGE KWA MADAI YA KUDHALILISHWA BUNGENI NA MBUNGE MMOJA WA CCM KUWA WANAPEWA VITI HIVYO KWA KUWA NA MAHUSIANO NA VIONGOZI WAO WA JUU.

WABUNGE HAO WALIOMBA MUONGOZO KWA NAIBU SPIKA LAKINI HAWAKUSIKILIZWA NDIPO WALIPOSIMAMA WOTE NA NAIBU SPIKA KUWATAKA KUKAA CHINI NA KUAMUA KUSUSIA KIKAO HICHO CHA BUNGE.
 
 WABUNGE HAO WAMEAMUA KUTOKA NNJE HUKU WAKIAHIDI KUJA NA TAMKO KALI KUHUSU UDHALILISHAJI WALIOFANYIWA.

MBUNGE WA KAWE NA MWENYEKITI WA UMOJA WANAWAKE CHADEMA, HALIMA MDEE AMESEMA KAULI ALIYOTOA NA MBUNGE WA JIMBO LA ULANGA GOODLUCK MLINGA KUZUNGUMZA BUNGENI KUWA WABUNGE WA CHADEMA ILI WAPATE UBUNGE WA VITI MAALUMU LAZIMA WAWE NA MAHUSIANO NA VIONGOZI WAO NI LA UDHALILISHAJI.
 






NA:JACKTAN MSAFIRI

No comments:

Powered by Blogger.