Header Ads

Breaking News
recent

YALIYOJILI WIKI JANA TABORA TANGA NA DAR ES SALAAM



TUANZIE KULE MKOANI TABORA

WANANCHI KATIKA KIJIJI CHA IGOMBE WILAYANI KALIUA MKOANI TABORA WAMEMLALAMIKIA MWENYEKITI WA SERIKALI YA KIJIJI HICHO NA MTENDAJI WAKE,PAMOJA NA KAMATI YA UJENZI WA VYUMBA VITATU VYA SHULE YA MSINGI KWA KUTAFUNA FEDHA AMBAZO WALIKUWA WAKICHANGA KWA AJILI YA UJENZI,NA KUWAACHA WANAFUNZI WAKISOMA CHINI YA MITI.

 

WAKIONGEA KATIKA MKUTANO WA HADHARA ULIOITISHWA NA MKURUGENZI HUYO KWA LENGO LA KUSOMEWA TAARIFA YA MKAGUZI WA NDANI JUU YA MICHANGO YA WANANCHI, WANANCHI HAO WAMESEMA WANAFUNZI WANAKABILIWA NA CHANGAMOTO KUBWA YA KUNYESHEWA MVUA.



AKISOMA TAARIFA HIYO MKAGUZI WA NDANI WA HALMASHAURI HIYO BW: JAFARI MTANGI AMEBAINISHA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI MBILI MIFUKO KUMI YA SARUJI, KUTAFUNWA NA UONGOZI WA KAMATI YA UJENZI, AMBAPO MTENDAJI ALIKUWA AKIWATOZA FEDHA WANANCHI BILA KUWAPA STAKABADHI.



AKITOA MAAMUZI YA MKURUGENZI,MWAKILISHI WA MKURUGENZI DHIDI YA WATUHUMIWA HAO WATENDAJI WAWILI WA KIJIJI HICHO MWAKILISHI BW:JOSEPHAT NGAZIME AMEWASIMAMISHA KAZI WAWILI NA KUMWACHIA MKUU WA WILAYA MAAMUZI DHIDI YA MWENYEKITI AMBAYE WANANCHI WALITAKA ATOLEWE MARA MOJA.


 TUELEKEE KULE TANGA

WATU WANNE WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAMEUWAWA NA WENGINE WAWILI WAMEJERUHIWA WAKATI WAKIRUSHIANA RISASI NA POLISI JIJINI TANGA
 
AKITHIBITISHA KUTOKEA KWA TUKIO HILO KAMANDA WA POLISI MKOA WA TANGA BW: LEONARD PAUL AMESEMA TUKIO HILO LIMETOKEA ENEO LA AMBONI LILILOPO NJE KIDOGO YA JIJI HILO IKIWA NI MKAKATI WA POLISI KUTHIBITI VITENDO VYA UJAMBAZI.
 
MAJAMBAZI HAO BAADA YA KUUWAWA WALIKUTWA WAKIWA NA VIFAA MBALIMBALI VILIVYOTAMBULIWA KWENYE MAENEO WALIOFANYA MATUKIO YA UHALIFU.
 

KAMANDA PAUL AMESEMA JESHI LA POLISI LINAENDELEA NA MSAKO MKALI TANGU KUTOKEA KWA MATUKIO MAWILI YA UJAMBAZI LIKIWEMO LA KUUWAWA KWA RAIA WANNE NA WENGINE WAWILI KUJERUHIWA VIBAYA KWA KUPIGWA RISASI APRIL 24 MWAKA HUU.

NA TUHITIMISHE NA DAR ES SALAAM

WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO IMESEMA INASIKITISHWA NA INALAANI VIKALI TUKIO LA KUUAWA KWA KUCHINJWA, MWANAMKE OLIVER ERASTO (23) NA MTOTO WAKE EMMANUEL (3), WAKAZI WA ENEO LA ZINGA, KATA YA DUNDA, WILAYANI BAGAMOYO, KUTOKANA NA WIVU WA KIMAPENZI.


WIZARA INAKEMEA MAAUJI HAYO, YANAYODAIWA KUTEKELEZWA NA FROWIN MBWALE  MKAZI WA KAWE, DAR ES SALAAM, AMBAYE NI MME WA MAREHEMU.


WIZARA HIYO IMESEMA MAUWAJI HAYO  YAMESABABISHA KUKATISHA MAISHA YA MAMA NA MTOTO, KATIKA KIPINDI AMBACHO TAIFA LINAHIMIZA UZINGATIAJI WA MCHANGO NA HAKI ZA WANAWAKE KATIKA MAENDELEO YA TAIFA, NA MWITIKIO WA HAKI YA KUISHI YA MTOTO KATIKA MIPANGO NA PROGRAMU ZA MAENDELEO ENDELEVU.
 
WIZARA INASISITIZA KUTAMBUA KUWA JUKUMU LA ULINZI NA USALAMA WA WANAFAMILIA LIKO MIKONONI MWA KILA MWANANCHI, HIVYO JAMII INAWAJIBU WA KUSAIDIA UDHIBITI WA UKATILI NA MAUAJI KATIKA FAMILIA NA JAMII . 


AIDHA WIZARA INAITAKA JAMII ITAMBUE KUWA HAKUNA MWENYE HAKI YA KUKATISHA UHAI WA MTU MWINGINE, NA MWANAMKE NA MTOTO ANAHAKI YA KUTHAMINIWA UTU WAKE, BILA UBAGUZI WOWOTE AMBAO UNAWEZA KUKATISHA MAISHA YAO.


WAKATI HUO HUO MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM IMETUPILIA MBALI RUFAA ILIYOKATWA NA MKURUGENZI WA MASHTAKA (DPP) ILIYOKUWA IKIPINGA KUONDOLEWA KWA SHITAKA LA 8 LA UTAKATISHAJI FEDHA LINALOMKABILI ALIYEKUWA KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA) HARRY KITILYA NA WENZAKE WAWILI.
 
UAMUZI HUO UMETOLEWA JIJINI DAR ES SALAAM NA JAJI MFAWIDHI WA MAHAKAMA HIYO, MOSES MZUNA ALIPOKUWA AKITOA MAJIBU YA RUFAA ILIYOKUWA IMEKATWA NA DPP.

AIDHA JAJI MZUNA AMEFAFANUA KUWA HATA KAMA AMEFUTA RUFAA HIYO LAKINI UPANDE WA JAMUHURI BADO UNA NAFASI YA KUBADILISHA SHITAKA AU HATI NZIMA YA MASHTAKA INAYOWAKABILI WASHTAKIWA HAO.
 

KWA UPANDE WAKE WAKILI MKUU WA SERIKALI TIMONY VITALIS AMEKUBALIANA NA UAMUZI ULIOTOLEWA NA MAHAKAMA HIYO JUU YA PINGAMIZI LAKE INGAWA BADO ANASIMAMIA WATUHUMIWA KUTOFUTIWA SHITAKA LA UTAKATISHAJI WA FEDHA.
 
NAYE WAKILI WA UTETEZI MAJULA MAGAFU AMESEMA KUWA WAO WANASUBIRI MAAMUZI YATAKAYOTOLEWA NA WAKILI WA SERIKALI ILI WAJUE NAMNA YA KUIKABILI KESI HIYO.
 



NA:JACKTAN MSAFIRI

No comments:

Powered by Blogger.