PLUIJM AKUBALI KUBAKI YANGA KAMA MKURUGENZI WA UFUNDI,TFF YAMSHIKA PABAYA KIJEBA WA CONGO-BRAZZAVILLE ‘AKIMBIA KIPIMO CHA UMRI CAF’.
Karibu
uweze kusoma habari mbalimbali za michezo zilitokea katika juma
lililoisha ambazo huwa zinarushwa na kituo cha redio cha 98.1 kwaneema
fmkila jumapili kuanzia saa tisa alasiri kwenye kipindi cha MICHEZO JUMA
HILI
PLUIJM AKUBALI KUBAKI YANGA KAMA MKURUGENZI WA UFUNDI
ALIYEKUWA kocha wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm amekubali kubaki klabuni kama Mkurugenzi wa Ufundi na ndiye atamshauri kocha mpya, George Lwandamina kuhusu muundo wa benchi la Ufundi.
Habari za ndani kutoka Yanga zinasema kwamba Pluijm amekubali kubaki katika klabu kama Mkurugenzi wa Ufundi baada ya mazugumzo na uongozi wiki hii.
Na kwa mujibu wa chanzi cha habari, Pluijm atakuwa na kikao na kocha mpya hivi karibuni, Mzambia Lwandamina kushauriana naye juu ya muundo wa benchi la Ufundi.
Kuna uwezekano mkubwa waliokuwa Wasaidizi wa Pluijm ndiyo wakawa wasaidizi wa Lwandamina pia, kwa kuwa wote bado wana mikataba na hakuna shaka juu ya utendaji wao.
Lwandamina, beki wa zamani wa kimataifa wa Zambia aliyezaliwa Agosti 5, mwaka 1963 yuko Dar es Salaam tayari baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili na anatarajiwa kuanza rasmi kazi mwishoni mwa mwezi huu.
Wachezaji wa Yanga wamepewa likizo hadi Novemba 28 na kwa sasa Lwandamina anaandaa programu yake ya mazoezi.
Kuhusu usajili wa dirisha dogo, ripoti ya kocha Pluijm ndiyo inasubiriwa ili kama imependekeza mchezaji wa kusajiliwa ifanyiwe kazi kwa kumshirikisha na kocha mpya.
Pluijm mwenyewe hakuwa tayari kuzungumza chochote kuhusu mustakabali wake Yanga akisema; “Siko tayari kuzungumza chochote kuhusu mustakabali wangu kwa sasa na sitakuwa kuwa sehemu ya tetesi zinazoendelea,”.
Hii ni awamu ya pili Pluijm kufundisha Yanga baada ya awali kufundisha kwa nusu msimu mwaka 2014, akimpokea Mholanzi mwenzake, Ernie Brandts kabla ya kwenda Uarabuni.
Alikwenda Al Shoalah FC ya Saudi ya Arabia na nafasi yake ikachukuliwa na Mbrazil, Marcio Maximo ambaye naye alifanya kazi kwa nusu msimu kabla ya Pluijm kurejeshwa Januari mwaka jana.
Saudi Arabia ambako alikwenda na aliyekuwa Msaidizi wake, Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa – Pluijm aliondoka baada ya kutofautiana na uongozi wa timu uliotaka kumsajilia wachezaji asiowataka.
Pluijm anaondoka Jangwani baada ya kuiongoza Yanga katika jumla ya mechi 128, akishinda 80, sare 25 na kufungwa 23.
Katika mechi 19 za nusu msimu mwaka 2014, alishinda 11, sare sita na kufungwa mbili, wakati katika mechi 110 za tangu mwaka jana, alishinda 69, sare 19 na kufungwa 21.
Msimu uliopita ulikuwa mzuri zaidi kwake, akibeba mataji yote matatu, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation (ASFC).
Pluijm pia aliiwezesha Yanga kufika hatua ya makundi ya michuano ya Afrika (Kombe la Shirikisho) kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1998 na mara ya pili kihistoria. Yanga ilifika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho mwaka huu baada ya mwaka 1998 kufika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.
Na kwa mafanikio hayo, haikuwa ajabu Pluijm akishinda tuzo ya kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwishoni mwa msimu uliopita.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilimkatia Rufaa CAF Langa Lesse Bercy baada ya kujiridhisha amevuka umri wa kucheza mashindano ya U-17.
Na hiyo ilifuatia Kongo- Brazzaville kuitoa Tanzania, Serengeti Boys katika hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania fainali za U-17 Afrika mwakani nchini Madagascar.
Kutokana na rufaa hiyo, Langa Lesse Bercy alitakiwa na CAF kufika makao makuu ya shirikisho hilo, Cairo, Misri kwa ajili ya kurudia na kuthibitisha umri wake kwa kipimo cha MRI (Magnetic Imaging Resonance).
Na TFF ilikubali sharti la CAF kugharamia zoezi zima ikiwa ni pamoja na kulipia gharama za usafiri wa mchezaji husika na daktari wake pamoja na kulipia gharama za vipimo.
Wakati zoezi la vipimo limepangwa kufanyika leo, Shirikisho la Soka la Kongo- Brazzaville limetoa taarifa kwamba Langa Lesse Bercy hataweza kutokea kwa sababu ambazo ziko nje ya uwezo wao.
Zoezi limepangwa kufanyika leo kuanzia Saa 5.00 asubuhi mjini Cairo, Misri. Ujumbe wa TFF wa watu wanne ukiambatana na madaktari wawili uliwasili mjini Cairo tangu Novemba 17, 2016 ili kuwa shuhuda wa zoezi la kipimo hicho.
Na jana usiku saa 5.00 TFF ilipokea ujumbe kutoka CAF kuwa mchezaji Langa Bercy ameshindwa kusafiri kwenda Cairo kwa kuwa yuko katika eneo lililoko “vitani”,eneo hilo halikutajwa.
Taarifa ya TFF kwa vyombo vya Habari leo, imesema kwamba wanaendelea kufuatilia kwa karibu jambo hili ili kuhakikisha haki inatendeka .

TFF YAMSHIKA PABAYA
KIJEBA WA CONGO-BRAZZAVILLE ‘AKIMBIA KIPIMO CHA UMRI CAF’
Mchezaji wa timu ya
taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Kongo- Brazzaville, Langa Lesse
Bercy ameshindwa kuwasili Cairo, Misri kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na
uchunguzi juu ya umri wake kama alivyotakiwa na Shirikisho la Soka Afrika
(CAF).

No comments: